Mhe Neema Lugangira (Mb.) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani akitoa Mafunzo ya Lishe Bora kwa Madiwani Viti Maalum |
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Hajat Faiza kulia akichukua dondoo kwenye Mafunzo ya Lishe Bora na Madiwani Viti Maalum wa Mkoa wa Kagera |
MADIWANI wa Viti Maalumu wapatao 64 kutoka Mkoani Kagera wamepatiwa mafunzo ya Lishe Bora kuhusu umuhimu wake na madhara yake ikiwemo ya kiuchumi iwapo hawatazingatia .
Mafunzo hayo yametolewa na Shirika la Agri Thamani yakiwa na lengo la kuwaelimisha kwa kina madiwani hao wanawake kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito, mama anaenyonyesha, mtoto chini ya miaka 5, kijana balehe, wanaume na wazee n.k.
Aidha madiwani hao pia walipata uelewa pia juu ya hali ya lishe nchini, madhara yake katika uzalishaji, jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali, malengo ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 na wajibu wao kama viongozi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani, Mhe Neema Lugangira (Mb) alisema kwamba baada ya mafunzo hayo wanategemea kuona bajeti ya lishe ikiongezwa na kutolewa.
Alisema bajeti hiyo itakapotolewa itumike kwa ajili ya afua za lishe zinazokubalika na hilo linawezekana sababu Madiwani Viti Maalumu wanashiriki vikao vinavyopitisha bajeti za Halmashauri na hivyo itakuwa rahisi kwao kuweza kuitetea na kuifuatilia.
Kwa upande wao Madiwani waliazimia kuanza na ajenda kuu tano ambazo ni kujua hali za lishe za wilaya zao, utengaji wa bajeti ya lishe, kujua aina za afua za lishe zinazokubalika, utendaji wa kamati za lishe na utekelezaji wa mikataba ya lishe iliyosainiwa kati ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya zao.
0 comments:
Post a Comment