Sunday, 13 December 2020

JAMAA AZUA GUMZO AKIMVISHA PETE MHUDUMU 'LIVE' KILABUNI BAADA YA KUPAPASWA

...

Jamaa mmoja aliyekuwa akijivinjari na wenzake kilabu moja mtaani Ngolida, Kiambu nchini Kenya amewavunja mbavu alipoamua kumvisha pete mhudumu wa kilabu hicho aliyempapasa.

 Lofa aliwaambia wenzake kwamba tangu aaanze kuwa na uhusiano na wanawake, hamna mwanamke aliyejua kumpapasa kiustadi kama dada huyo. 

“Katika maisha yangu sijawahi kuhisi nilivyohisi mwanadada huyu aliponipapasa,” lofa alisema bila kufafanua kwa mujibu wa Taifa leo.

 Duru zinaarifu kwamba jamaa alisimama mbele ya wateja wengine, akamkumbatia mrembo huyo na kumpiga busu moto moto kabla ya kutoa pete na kutaka kumvisha.

 “Kuanzia leo hautafanya kazi katika kilabu hiki. Ulifanya kitu ambacho sijawahi kufanyiwa na mwanamke mwingine",alisema. 

Penyenye zinasema shangwe na nderemo zilisikika kilabuni humo baada ya Mrembo huyo kuikubali pete ya jamaa huyo. 

“Wanawake wengine wangekuwa sampuli yako ningekuwa ninahisi vizuri. Sasa wengine wanaonimezea mate watajipanga. Nitakuoa uwe mke wangu na nitakutunza vizuri,” jamaa aliongeza.

 Penyenye zinasema mwanadada aliondoka akilengwa lengwa na machozi ya furaha huku wateja wakiachwa midomo wazi. 

“Mungu ni wa maajabu. Nimeishi kwa miaka mingi na hakuna mwanamume aliyejitolea kunivisha pete. Nioe tu hata kama una mke mwingine sitajali,” mrembo alisema. 

Duru zinaarifu kwamba barobaro ambaye pia alishindwa kuficha furaha yake hadi akawanunulia watu waliokuwa karibu na meza yake pombe.

 Baadaye ilifichuka kwamba mrembo huyo alikuwa amempakulia lofa asali mara kadhaa kabla ya tukio hilo. Hata hivyo haikujulikana iwapo uhusiano wa wawili hao uliendelea baada ya kioja hicho.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger