Baba yake mzazi na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, Mzee Urban Costa Ndunguru, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 19, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu.
Jokate amesema kuwa mzee wake amefikwa na mauti hayo, baada ya kuugua kiharusi na alikuwa amelazwa kwenye chumba cha uangalizi maalum yaani ICU.
“Alilazwa kwa muda katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU), alikuwa akisumbuliwa na kiharusi leo alfajiri amefariki dunia,” amesema Jokate.
Jokate amesema taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Oysterbay.
0 comments:
Post a Comment