Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akihutubia kwenye Mahafali ya Shule ya Awali ya Al Wafaa inayo milikiwa na Taasisi ya Dhi Nureyn iliyopo eneo la Mandewa yaliyofanyika jana mkoani hapa.
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akikabidhi vyeti kwenye Mahafali ya Shule ya Awali ya Al Wafaa inayo milikiwa na Taasisi ya Dhi Nureyn iliyopo eneo la Mandewa yaliyofanyika jana mkoani hapa. Kutoka kulia ni Sheikh wa Wilaya ya Singida, Issa Simba, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mikidadi Abrahman na kushoto ni mmiliki wa shule hiyo, Hamisi Ntandu,
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akikabidhi vitabu kwenye Mahafali hayo.
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau akikabidhi vitabu kwenye Mahafali hayo.
Wanafunzi wakiwa na vitabu walivyo kabidhiwa baada ya kufanya vizuri kwenye masomo ya dini.
Wanafunzi wakiwa na vitabu walivyo kabidhiwa baada ya kufanya vizuri kwenye masomo ya dini.
Mmiliki wa shule hiyo, Hamisi Ntandu, akiwa kwenye Mahafali hayo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Msingi na Awali Mikidadi Abrahman, akisoma risala kwenye mahafali hayo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
KATIBU wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Buruan Mlau anewapongeza Waislamu mkoani hapa kwa kuwa na muamko wa kujenga shule kwa ajili ya watoto wao.
Mlau ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa pongezi hizo kwenye mahafali ya Shule ya Awali ya Al Wafaa inayo milikiwa na Taasisi ya Dhi Nureyn iliyopo eneo la Mandewa yaliyofanyika jana mkoani hapa.
"Katika Mkoa wa Singida hivi sasa tuna shule za kiislamu sita tunakila sababu ya kumshukuru mwenyezi Mungu kwani hapo zamani hatukuwa na shule hata moja tulikuwa nazo katika mikoa ya Mwanza, Arusha , Dar es Salaam na mikoa mingine." alisema Mlau.
Mlau aliwapongeza sana waislamu hao kwa ushirikiano mzuri wanaoufanya wa kujenga shule ili watoto wao waweze kupata elimu zote mbili kwa maana ya dini na elimu ya dunia.
Aidha Mlau aliwataka waislamu hao kuendelea kushirikiana na kuziboresha shule hizo kwa ajili ya manufaa ya watoto wao.
Akizungumza katika mahafali hayo Sheikh wa Wilaya ya Singida, Issa Simba alisema hata Mtume Muhammad aliwahi kuzungumza kuwa mwanadamu yeyote akitaka kuishi maisha mazuri duniani na peponi ni lazima awe na elimu na si vinginevyo.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Msingi na Awali Mikidadi Abrahman alisema ilisajiliwa mwaka Januari 21, 2018 kwa namba ya usajili EL17536 kuwa shule ya mchanganyiko ya wavulana na wasichana na kuwa Januari 6, 2018 walipatiwa kibali kwa ajili ya shule ya bweni na kuwa sasa wanatoa elimu kuanzia ya awali hadi darasa la saba.
Alisema kwa sasa wana jumla ya wanafunzi 335 wakiwemo wavulana 173 na wasichana 162 na walimu 20, walimu 13 wakiume na saba wa kike.
Abrahman alisema kati ya walimu hao sita wanafundisha masomo ya dini na 14 masomo ya kawaida kwa maana elimu ya mazingira.
Alisema baadhi ya malengo ya kuanzisha shule hiyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu kwa kutoa elimu bora yenye tija kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment