Mama mzazi wa mshereheshaji Emmanuel Matebe maarufu kama MC Pilipili, Mariam Matebe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 20, 2020, kwa ajali ya gari wakati akielekea ukumbini kwenye harusi ya mtoto wake maeneo ya Afrikana Jijini Dar es Salaam.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram MC Pilipili ameandika maneno haya, “Ulale salama mama yangu mpenzi Mariam Matebe, umetufundisha upendo na umefariki ukijariibu kuonesha upendo lala salama mpenzi“.
Kwa mujibu wa familia mwili wa marehemu Mama MC Pilipili utasafirishwa leo jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu Jijini Dodoma kwa ajili ya taratibu za maziko.
0 comments:
Post a Comment