Wasanii watakaofanya show leo Jumatano katika Tamasha la Wasafi Festival nchini Kenya kutoka Tanzania wamepokewa kwa shangwe kubwa na Wakenya hapo jana.
Awali show hiyo iliingiwa na sitofahamu baada ya msanii Diamond na Rayvanny kutoruhusiwa kufanya onesho nje ya nchi baada ya kufungiwa na BASATA kwa kosa la kuimba wimbo Mwanza ambao ulifungiwa na baraza hilo.
Lakini juzi baraza hilo lilitoa ruhusa kwa waimbaji hao ya kufanya enesho kwa madai adhabu ya kufungiwa ilikuja kwa wawili hao wakati tayari wameshaingia makubaliano ya enesho la Kenya.
Baada ya team hiyo kuwasili nchini Kenya, Rais wa WCB Diamond Platnumz aliwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwaajili ya enesho hilo la aina yake.
0 comments:
Post a Comment