Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania ATCL Ladislaus Matindi, ameeleza tayari ameshamkabidhi Rais Magufuli orodha ya majina ya viongozi ambao walikatisha safari zao za ndege katika shirika hilo licha ya kukatiwa tiketi za serikali.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amedai wameshatekeleza agizo hilo la Rais Magufuli ambalo alilitoa kwenye hafla ya upokeaji wa ndege mpya ya Tanzania A220-300 aina ya Airbus.
Matindi amesema “majina ya vigogo husika tumeshayakabidhi kwa Rais, tangu tumeelekezwa tulifanyia kazi maelekezo hayo na kisha tukayakabidhi sehemu husika,”
“Siwezi kutaja ni vigogo wa kada gani, wasiliana na Ofisi ya Rais wataweza kuwa na majina pamoja na Idara au Taasisi wanazotoka, sisi tumepeleka orodha,” ameongeza Luhindi.
Akizungumza Desemba 23, 2018 Rais Magufuli alisema “nimeambiwa pia baadhi ya tiketi huwa zinakatwa na watendaji wa serikali halafu wakati wa mwisho hawasafiri, anatakiwa kusafiri kwenye ndege na amekatiwa tiketi na serikali, lakini hasafiri, hivyo kwa nafasi ile ndege inaenda tupu,” Viongozi wanaokatwa mishahara wafika kwa Magufuli.
Chanzo:Eatv
0 comments:
Post a Comment