Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City Jumapili hii hivyo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amewaomba wanachama kuichangia timu ili iweze kufafiri kwa ndege na kiasi kitakachopelea yeye ataongezea.
Zahera ambaye hayupo nchini amedai kitendo cha timu kusafiri tarehe 27 na kwenda kucheza tarehe 29 sio rahisi kwenda kwa basi hivyo ni lazima iende kwa ndege ili iweze kupata matokeo.
''Mimi kocha Mwinyi Zahera naomba wanachama waichangie klabu iweze kusafiri kwa ndege kwenda Mbeya ili tukacheze na tupate matokeo na mimi binafsi nitaongezea kiasi kitakachopelea'', amesema Zahera.
Aidha Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo amesema matokeo ya Yanga ni muhimu kwa wanachama na timu nzima ili kuendelea kuongoza ligi kwahiyo kila mmoja anayo sababu ya kuhakikisha timu inasafiri vyema.
Yanga kwasasa inaongoza ligi ikiwa na alama 47 kwenye mechi 17 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 40 kwenye mechi 16 huku Simba ikiwa nafasi ya 3 na alama 30 kwenye mechi 13.
Chanzo: Eatv
0 comments:
Post a Comment