Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB) inautaarifu umma kuwa imesitisha mikopo ya elimu ya juu
iliyokuwa ikitolewa kwa walimu-wanafunzi
wanne waliosimamishwa masomo
kwa kuhusika katika tukio la kumshambulia na kumuumiza mwanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya. Walimu hao walikuwa katika mafunzo
ya vitendo.
1. Frank Msigwa - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
2. John Deo- Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
3. Evance Sanga - Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE)
4. Sante Gwamaka - Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
Kwa utovu huo wa nidhamu, wanafunzi hao
wamesimamishwa masomo na mamlaka husika kwa hiyo wamepoteza sifa za
kuendelea kupokea mikopo. Mikataba inayosainiwa na wanufaika wa mikopo
inawataka wanufaika kuzingatia masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na
nidhamu na kufuata sheria na taratibu za vyuo na mamlaka halali.
Aidha, kwa mujibu wa taratibu za kukopeshwa, wanafunzi hawa watatakiwa kuanza kurejesha kiasi walichokopeshwa mara moja.
Bodi ya Mikopo inawakumbusha wanufaika
wanaoendelea masomo kuzingatia masharti ya ukopeshwaji na kuheshimu
sheria, kanuni taratibu na kuwa mfano mwema katika jamii. Mikopo na
ruzuku zinazotolewa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaandaa kuwa raia
wema, waadilifu, na wachapa kazi ili kujenga uchumi imara na ustawi kwa
wote.
Imetolewa na:
Abdul-Razaq Badru
Mkurugenzi Mtendaji
Ijumaa, Oktoba 7, 2016
0 comments:
Post a Comment