Mwalimu
Israel Mlowasa (40) wa Shule ya Sekondari Nkuhungu katika Manispaa ya
Dodoma, amekutwa ameuawa nyumbani kwake na kiganja chake cha mkono wa
kulia kukatwa na kuondoka na wauaji hao.
Taarifa
iliyotolewa na Jeshi la Polisi inasema kwamba mauaji hayo yamefanyika
juzi maeneo ya Chang’ombe Extension katika Manispaa ya Dodoma.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Nkuhungu, Fidelis Kaishozi alisema mwalimu
huyo alipotea tangu Oktoba 2, mwaka huu na taarifa kutolewa Polisi.
Imeelezwa kuwa maiti ya mwalimu huyo ilikutwa katika pagala la nyumba eneo la Nkuhungu.
Hakuna
mtu aliyekamatwa kuhusu mauaji hayo, msako mkali unaendelea ili kubaini
wahusika na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Dodoma
kwa uchunguzi zaidi wa madaktari.
0 comments:
Post a Comment