TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
TANGAZO
KWA UMMA
Tume ya
vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa imekamilisha kuchakata maombi ya kujiunga na Vyuo Vikuu
na Taasisi za Elimu ya Juu kwa awamu ya kwanza na ya pili. Orodha na
majina ya walichaguliwa yameshapelekwa
vyuoni kwa ajili ya kuiidhinishwa na Seneti za vyuo husika. Baadhi
ya vyuo vimeshaanza kuyatangaza.
Hata hivyo, kuna waombaji ambao bado wako kwenye mfumo na hawajachaguliwa kwenye kozi yoyote
kati ya walizoomba kutokana na sababu
mbalimbali kama ifuatavyo:-
·
Ushindani mkubwa katika programu za masomo
walizoomba ukilinganisha na ufaulu
wao;
·
Waombaji kushindwa kukamilisha taratibu za
uombaji; na
·
Waombaji kutokuwa na sifa kwa kozi walizoziomba.
Kutokana na
hali hiyo, Tume inautangazia umma kuwa mfumo wa udahili utafunguliwa tena kwa awamu ya tatu mnano tarehe 10
mpaka tarehe 16 Oktoba 2016 ili
kuruhusu waombaji na aina hii kufanya uchaguzi upya au kukamilisha maombi yao.
Tume
inapenda kufafanua kuwa programu za masomo zisizoonekana kwenye mtandao zimekwishajaa, hivyo waombaji watalazimika
kuomba zile tu zinazoonekana mtandaoni.
Zoezi hili
la uombaji kwa awamu ya tatu linawahusu waombaji wenye sifa za kidato cha Sita, Stashahada na sifa
linganishi. Hakutakuwa na malipo yoyote kwa
waombaji hawa. Tume inapenda kisisitiza kwamba, awamu hii haitawahusu waombaji wapya, ambao
hawakuwahi kujisajili wala kuomba udahili kwa
awamu ya kwanza na ya pili.
Imetolewa na Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 10/10/2016
0 comments:
Post a Comment