IJUMAA iliyopita ilikuwa ni siku kubwa
ingawa haikuwahi kuwekwa katika kalenda hapo kabla. Ilikuwa ni siku
ambayo umma kwa upana wake, ulitambua jinsi gani sekta ya usafirishaji
ilivyo muhimu. Nina uhakika, mamia ya watu walipata hasara ya mamilioni
ya shilingi.
Wananchi wakilala chini kuepuka athari za mabomu ya machozi.
Hii ilitokana na mgomo wa madereva wa mabasi ya mikoani na daladala.
Chanzo ni wito wa serikali wa kuwataka madereva hao kurejea shule,
katika…

katika harakati za kudhibiti ongezeko kubwa la ajali za barabarani
zinazoua mamia ya abiria kila mwaka.Historia, inaonyesha migomo ni silaha ya mwisho inayotumiwa na watu wanaoamini hawatendewi haki na mamlaka zilizo juu yao. Lakini wakati wao wakifanya migomo kwa ajili ya kudai wanachoamini ni stahiki yao, mamia kwa maelfu wanaoathirika, ni wasio na hatia kabisa.
Ingawa kiasili migomo ni haki na inatokea kila mara sehemu mbalimbali duniani, hapa kwetu, imekuwa sehemu ya maisha katika miaka ya karibuni. Sekta nyingi zinagoma kwa madai mbalimbali, lakini mgomo mbaya zaidi kuliko huu wa juzi, ni ule wa madaktari uliosababisha vifo vya ndugu, jamaa na wapendwa wetu wengi.
Ingawa migomo siku zote ni mibaya kwa sababu wanaoathirika siyo walengwa, lakini angalau inatoa ishara kwa wenye mamlaka juu ya kuamka kwa wanaogoma.
Na mamlaka yenye kufikiri chanya, ni lazima izione dalili hizi kama zisizo njema kwake, kwa sababu migomo huambukiza, kutoka sekta hadi sekta, idara hadi idara, jamii hadi jamii na mwisho, mtu hadi mtu. Inapotokea kila kada ya watu kuamini kuwa mgomo ndilo suluhisho pekee la matatizo yaliyo mbele yake, kitu cha ukweli cha kukitaraji, ni anguko kubwa!
Ni wakati wa mamlaka kujifunza, kutoka mgomo mmoja hadi mwingine. Mara nyingi makosa ya mamlaka zetu huwa ni jinsi zinavyotoa majibu mepesi kwa maswali magumu na hili ndilo hasa linalotoa hamasa ya kufanyika kwa migomo.
Kuna watu kule kwenye mamlaka zetu wanadhani wao wana akili kuliko tulio mitaani kiasi kwamba hata wanaposhauriwa vizuri, hawataki kusikiliza na kubakia na kauli dhaifu ya kuwa hii ni amri ya serikali, bila kujua kuwa sisi ndiyo serikali yenyewe na wao ni watumishi wetu tu!
0 comments:
Post a Comment