Sio siri, sote tunakubali kwamba serikali ya awamu ya nne ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufungua ukurasa wa uhuru wa habari, utawala bora wa sheria na kuheshimu haki za binadamu, nchi yetu imekuwa iking'ara katika kudumisha haki za kidemokrasia.
Kwa upande wa kimataifa na utawala bora Tanzania imepiga hatua kubwa sihitaji kulizungumzia hilo kwa sanatunajua ugeni wa rais wa china na rais Obama pamoja na kuingia mikataba mikubwa ya maendeleo kwa nchi yetu.
Ikumbukwe kuwa April jana rais Kikwete alipata tuzo ya heshima ya kuwa rais mwenye mchango mkubwa kwa nchi yake barani Africa kwa mwaka 2013. Tuzo hiyo ya heshima ilitolewa na jarida maarufu la African Leadership Magazine Group, Mjini Washington Dc ilipokelewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Mhe Bernard Membe.
Tuzo hizo hutolewa kila mwaka kwa viongozi wa Africa wenye mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii.
Kwa watanzania tuliowengi rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kuwa mstahamilivu, shupavu mwenye msimamao na mpenda haki na asiyechukua maamuzi ya kukurupuka kwa maneno ya vijiweni ambayo mengi ni uzushi na uongo yenye kuleta uchonganishi baina wananchi na serikali yao walioichagua.
0 comments:
Post a Comment