Wednesday 27 February 2019

WAZIRI MWAKYEMBE AAGIZA DUDUBAYA ACHUKULIWE HATUA KWA KUMDHIHAKI MAREHEMU RUGE


Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe amelielekeza Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua Msanii Dudu Baya kwa kumdhihaki Marehemu Ruge Mutahaba. 

Tangu kutokea kwa taarifa za kifo cha Ruge jana, Dudubaya amekuwa akitoa maneno mtandaoni kumdhihaki Ruge akimtuhumu kuwa enzi za uhai wake alikuwa mnyonyaji wa wasanii.

Dudubaya amepost vipande vya video katika mtandao wa Instagram akimdhihaki Marehemu Ruge ANGALIA <<HAPA>>

Share:

WALIOIGIZA SAUTI YA RAIS NA KUTAPELI WAKAMATWA


Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni Mwenyekiti wa Sameer Africa, aliigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara.

Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi huku vyombo vya habari nchini Kenya vikitofautiana kwamba ni shilingi milioni 10, huku gazeti lingine likiandika kwamba ni shilingi milioni 80.

“kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano ya simu”, ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation.

Wakati wa operesheni hiyo, polisi walikamata magari aina ya Toyota Land Cruiser, Toyota Mark X , Toyota Axio na Toyota Crown.

Uchunguzi huo unatarajiwa kubaini ikiwa magari hayo yana uhusiano na uhalifu huo.

Mpaka sasa Bwana Merali (aliyetapeliwa) na rais Kenyatta bado hawajazungumzia juu ya tukio la kukamatwa kwa watu hao.
Share:

MWANAFUNZI AUAWA KWA KUPIGWA NA KIRANJA SHULENI

 Hali ya majonzi imeikumba Shule ya Sekondari St Joseph Nyabigena iliyopo Gucha Kusini, Kaunti ya Kisii nchini Kenya kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao anayedaiwa kupigwa na kiranja.

 Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu anadaiwa kuaga dunia baada ya kukimbizwa katika Hospitali ya Wamisionari ya Tabaka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Nation, marehemu alianguka na kuzimia baada ya kupigwa na kiranja, na inadaiwa walizozana kabla ya kisa hicho asubuhi ya Jumanne 26,2019.

 “Marehemu alikuwa akisoma Bibilia kuelekea saa moja asubuhi. Baada ya mgogoro kidogo kati yao kiranja alimpiga kofi kisha teke la tumbo na hapo alianguka na kuzimia,” mmoja wa wanafunzi alisema.

 Usimamizi wa hospitali ulikataa kusema na wanahabari kuhusu kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

 Kamanda wa Polisi wa Kaunti Martin Kibet alithibitisha kutokea kisa hicho na kusema tayari uchunguzi wa polisi umeanzishwa. 

“Tunafahamu kuhusu kisa hicho na tumewaruhusu polisi kufanya uchunguzi wao kabla ya kutoa taarifa.” Kibet alisema.

 Mwalimu Mkuu Mathew Simiyu alitoweka katika shule hiyo mara baada ya tukio hilo na wanahabari hawakupata fursa ya kusema naye.

 Mwalimu ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema, mwalimu mkuu alizungumza na wanafunzi na kuwataka kuwa watulivu kabla ya kuondoka.

 Baadhi ya walimu waliozungumza na wanahabari waliwalaumu walimu wakuu kwa kuwapa mamlaka mengi viranja.

 “Waliohusika wakamatwe na kusema kilichotokea. Ni makosa kwa wanafunzi kupewa idhini ya kuwaadhibu wanafunzi wengine,” mmoja wa walimu alisema.

 Wanafunzi walisusia chakula cha mchana na kulalamika kuhusu viranja kuwafanyia ukatili shuleni. 

Maafisa wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Nyamarambe walimhoji mwalimu aliyekuwa zamu kuhusu tukio hilo lakini haikubainika iwapo yeyote ametiwa nguvuni kuhusiana na kifo cha mwanafunzi huyo.
Share:

FAMILIA YAZUNGUMZIKA KIFO CHA RUGE MUTAHABA

Familia ya Marehemu Ruge Mutahaba ambaye amefariki dunia hapo Jana nchini Afrika Kusini, imeweka wazi kilichotokea mpaka Ruge akakutwa na mauti, akiwa hospitali akiendelea na matibabu ya figo ambayo ilikuwa ikimsumbua.

Mombeki Barego ambaye ni ndugu wa Ruge Mutahaba amesema kwamba jana asubuhi Ruge aliamka huku presha yake ikiwa haiko sawa, lakini licha ya madaktari kufanya jitihada zao ili kumuweka sawa, ilishindikana na kusababisha kupoteza maisha.


“Asubuhi leo (jana) ndugu yetu Ruge Mutahaba, aliamka katika hali ambayo presha yake ilikuwa haijatulia, madaktari na wasaidizi wengine wa hospitali walijaribu kumsaidia, lakini mnamo saa 10:30 Jioni kwa saa za South Afrika au saa 11:30 kwa muda wa hapa nyumbani, ndugu yetu Ruge Mutahaba, alifariki akiwa na mdogo wake na watu wa dini ambao walikuwepo naye”,amesema Mombeki.


Mombeki ameendelea kwa kusema kwamba utaratibu wa kurudisha mwili wa marehemu unaanza kufanyika, huku akiwashukuru watu waliojitokeza kuifariji familia yao.


“Na kwa sasa familia inashukuru watu amabo wamefika hapa kutufariji kwa muda mfupi, na utaratibu wa kuangalia namna ya kumrudisha ndugu yetu nyumbani kwa ajili ya mazishi ndio zinaanza, kesho (leo) tutakuwa tunafahamu zaidi kuhusu huo utaratibu na kuweza kutoa taarifa rasmi ya utaratibu na mazishi”, amesema Mombeki.


Ruge Mutahaba alikuwa mmoja wa waasisi wa Clouds Media Group na mmoja ya watu aliochangia kukuza sanaa ya bongo kwa kuibua wasanii mbali mbali, na atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye maisha ya vijana wengi.


Ruge alianza kusumbuliwa na tatizo la figo mwishoni mwaka 2018 ambapo alilazwa katika hospitali ya Kairuki, na baadaye kuhamishiwa nchini Afrika Kusini ili kupata matibabu zaidi, mpaka kifo kilipomkuta Februari 26, 2019.
Share:

CCM YAMLILIA RUGE MUTAHABA



Share:

KIKWETE ATOA NENO KIFO CHA RUGE ' TUMEPOTEZA KIJANA MAHIRI'

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameeleza maumivu aliyonayo kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Kikwete ameandika ujumbe maneno yafuatayo:

“Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. 

"Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu.

"Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Namuombea kwa Mola ampe Mapumziko Mema Peponi. Ameen. "

Share:

BUHARI ATANGAZWA KUWA RAIS WA NIGERIA

Muhammad Buhari ametangazwa na Tume ya Uchaguzi Nigeria kuwa mshindi wa kiti cha Urais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Februari 23,2019

Buhari ameshinda kwa kura millioni 15 akiwa zaidi kwa kura millioni 4 zaid ya mpinzani wake Atiku aboubakar . Hata hivyo, Upinzani wamekataa matokeo hayo.


Chama cha Buhari kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.


Tume ya uchaguzi imesema kuwa itaangalia malalamiko yote kabla ya kutangaza Rasmi matokeo ya uchaguzi.
Share:

CHAMA CHA WAIGIZAJI KINONDONI ( KAMAMIKI ) CHAMLILIA RUGE

Chama cha Waigizaji Kinondoni, kimetoa pole zake kwa kifo cha  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba aliyefariki jana Jumanne Februari 26,2019.

Katika taarifa yao iliyosainiwa na  Mkuu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Masoud Kaftany imesema enzi ya uhai wake, Ruge alitoa mchango mkubwa kwa  wasanii wa muziki na fani zingine na kutoa elimu ya ujasiriamali

Pia alitoa mchango kwa Taifa la Tanzania katika nyanja ya muziki ambazo zilikuwa  chachu kubwa ya kujenga na kuandaa jamii ya Kitanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa na kijamii katika ujenzi wa taifa.

==>>Hii ni taarifa yao 
*Kamati ya Matukio Maadili na mikataba ya Chama cha Waigizaji ( M) Kinondoni ( KAMAMIKI ) Inatoa pole kwa *CLOUDS MEDIA GROUP na Familia Ya Marehemu *RUGE MUTAHABA* Kwa kuondokewa na Mpendwa Wetu Ruge Mutahaba ambaye Enzi za Uhai wake alikuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media

Enzi ya uhai wake *Ruge* alitoa mchango Mkubwa Kwa Wasanii wa Muziki na Fani zingine na kutoa Elimu ya Ujasirimali kwa Taifa La Tanzania Katika Nyanja Ya Muziki , ambazo Zilikuwa Chachu Kubwa ya Kujenga na Kuandaa Jamii ya Kitanzania Kukabiliana na Changamoto Mbali Mbali za Kimaendeleo , Kiuchumi , Kisiasa na Kijamii Katika Ujenzi wa Taifa.

Tunamuombea Kwa Mungu apumzike kwa Amani kwenye Nyumba Yake ya Milele. 

Bwana Ametoa , Bwana Ametwaa , Jina la Bwana Lihimidiwe . Inna Lillah wa Inna Illayhi Raj'uun. Asante. 

Imetolewa Na; Mkuu wa Idara ya Habari , Uenezi na Mahusiano na Umma - TDFAA ( KINONDONI ). *Masoud kaftany*
Share:

Tuesday 26 February 2019

NAPE,MWIGULU,SUGU,JANUARY MAKAMBA WAMLILIA RUGE


Kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kimewashtua wengi, miongoni ni wanasiasa ambao wametumia mitandao yao ya kijamii kuelezea hisia zao na kutoa salamu za pole.


Miongoni mwa wanasiasa waliomzungumzia Ruge ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba ameandika kwenye Twitter akisema, “Ruge. Ruge. Ruge. Nakosa maneno ya kutosheleza kuelezea maumivu na huzuni niliyonayo.”

“Kwa sasa, dua na fikra zangu ni kwa mama, Dk Mutahaba, ndugu na marafiki ambao walihangaika sana kuhakikisha anapona. Nikipata nguvu nitasema zaidi. Tangulia jamaa yangu, tunakuja. #RIPRuge.”

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameandika kwenye Instagram, “Sikutaka kuamini habari hii mpaka nimezungumza na Joseph Kusaga na kaniambia ni kweli umetutoka!”

“Pole sana kwa familia, Clouds Media Group, uongozi na wafanyakazi wote pamoja na wadau wote wa tasnia ya muziki na burudani tulioguswa na msiba huu mzito... R.I.P RUGE.”

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba ameandika, “Umeondoka Ruge Mutahaba, umeondoka shujaa, umeondoka mpambanaji.”

“Pole kwa familia, ndugu na jamaa, pole zaidi kwa Watanzania wote kwa msiba huu mzito.”

“Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika" Ayubu 42:2,” ameandika Mwingulu kwenye akaunti yake ya Instagram akiambatanisha na picha ya Ruge.

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameandika kwenye Twitter akisema, “Pumzika kwa amani kaka! Huna mfano wako duniani, maisha yako yameacha alama kubwa, utaishi milele kwa wema wako! Ndugu, Rafiki na mzalendo wa kweli!”

Mbunge wa Segerea (CCM), Bonnah Kamoli ameandika, “Pumzika kwa amani, kaka yetu Ruge Mutahaba, mchango wako kwenye jamii ni mkubwa sana na hautasahaulika.” 

“Mwenyezi Mungu awajalie familia, ndugu na wale wote walioguswa na msiba huu nguvu, hekima na busara.#RIPRuge,” ameongeza
Via Mwananchi
Share:

MAKAMU WA RAIS ATUA SHINYANGA...ATEMBELEA KITUO CHA AFYA SAMUYE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Shinyanga tayari kwa ziara ya kikazi ya siku 5.

Makamu wa Rais ambaye amesafiri kwa njia ya barabara akitokea mkoani Tabora ambapo napo alikuwa na ziara yenye lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo.

Mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga Makamu wa Rais alitembelea kituo cha Afya cha Samuye na kupata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.

“Serikali ina kila nia ya kusogeza huduma za afya bora kwa wananchi”alisema Makamu wa Rais.

Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inakuja na sheria ya mpango wa bima za afya kwa wote ambayo itamuhitaji kila mtanzania kuwa na bima ya afya.

Makamu wa Rais amewataka wakazi wa kata ya Samuye kushirikiana katika kuzuia mimba za utotoni kwani kwa kiasi kikubwa zinahatarisha maisha ya watoto wa kike.

Kwa upande wake Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara amesisitiza Halmashuri kutenga asilimia 40 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kumalizia maboma ya zahanati wakati serikali kuu inaleta pesa za kumalizia maboma ya shule na madawati.
Share:

RAIS MAGUFULI AMLILIA RUGE MUTAHABA....ATUMA SALAMU ZA POLE



"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina" - Rais Magufuli.


Share:

HATIMAYE MWILI ULIOKAA MOCHWARI MIEZI NANE WAZIKWA MBEYA

 Hatimaye mwili wa Frank Kapange (22) leo Jumanne Februari 26,2019 umechukuliwa na familia yake katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada ya kukaa mochwari miezi nane na siku 22.

Mwananchi lililokuwapo hospitalini limeshuhudia baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu walifika saa 3:30 asubuhi ambapo walichangishana fedha kwa ajili ya kusaidia shughuli za msiba.

Akizungumza hospitalini hapo, msemaji wa familia, Julius Kapange amesema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuamuliwa na Mahakama kuwa wazike ndani ya wiki moja la sivyo jiji lingezika.

“Leo tumefanikiwa kuchukua mwili wa kijana wetu, tunaenda kuzika kijijini kwetu Syukula Rungwe sababu ya kufanya hivyo ni kwamba Mahakama ilitutaka tuzike kabla ya wiki moja.”

“Hivyo tukaona ni vyema tufanye hivyo kuliko kuendelea kumtesa mwanetu lakini mpaka tumefika hatua hii Mahakama haijatutendea haki katika kuamua kesi yetu,” amesema Kapange.

Kapange amesema siku ya Jumapili ya Februari 24,2019 waliitwa na mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa ambapo waliambiwa wachukue mwili wa kijana wao na gharama za kuhifadhia maiti hiyo kwa muda wote wamesamehewa.
“Sisi tulienda mahakamani kuomba mwili wa mtoto wetu uchunguzwe kwani kifo chake kilikuwa ni cha utata na siyo kususia kama wengine wanavyosema na baada ya mazishi tutaendelea kufanya shughuli zingine za kimaendeleo,” amesema Kapange.

Akizungumza kwa njia simu mkurugenzi wa hospitali hiyo, Godlove Mbwanji amesema wameamua kusamehe gharama za kutunzia maiti hiyo kwa muda wote ili fedha ambazo waliziandaa zikatumike kwenye msiba.
Frank alifariki Juni 4, 2018 huku kifo chake kikigubikwa na utata kutokana na mazingira yake baada ya ndugu kudai kijana wao ambaye alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo za mitumba soko la Sido jijini Mbeya kufariki kwa kipigo akiwa mikononi mwa polisi hivyo ndugu waligoma kumchukua na kwenda kumzika.

Kutokana na ndugu hao kuona ukakasi wa kifo cha kijana wao walitaka kujiridhisha pasipo shaka juu ya kilichosababisha hivyo wakafungua shauri Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya itoe amri ya kufanyika kwa uchunguzi rasmi wa kisheria wa kifo cha kijana wao lakini mahakama hiyo Agosti mwaka jana ilitupilia mbali shauri hilo baada ya kuona kukosa mashiko na kuamuru mwili huo kuzikwa na ndugu wanahitajika kubeba gharama zote za mazishi.

Ndugu walidai kutoridhika na uamuzi huo, wakaamua kukataa rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambayo nayo Novemba 2018 ilitoa uamuzi wa kuifuta kesi hiyo baada ya kujiridhisha kwamba mlalamikaji hakufuata taratibu zilizopaswa wakati wa kufungua kesi hiyo.

Na Ipyana Samson, Mwananchi 
Share:

Breaking News : RUGE MUTAHABA AFARIKI DUNIA


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media group, Ruge Mutahaba amefariki dunia.
R.I.P Ruge.
Taarifa kamili inakuja hivi punde
Share:

SIMBA YAENDELEZA UBABE...YAIFYATUA LIPULI 3-1

Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Lipuli katika uwanja wa Samora umemalizika kwa Simba SC kuichapa Lipuli 3-1.
Share:

MTU NA DADA YAKE WAFARIKI KWA KUPIGWA SHOTI YA UMEME WAKIANIKA NGUO


Watu wawili wa familia moja, Zulfa Chami na Zuhura Chami wamepoteza maisha, baada ya kupigwa shoti ya umeme na kamba ya kuanikia nguo katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi.

Zulfa (24) na Zuhura (28) wamefikwa mauti hayo leo wakati wakianika nguo.

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadae kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Hamisi Issah zinaeleza kuwa ndugu hao wa familia moja walifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa shoti ya umeme.

"Ni kweli ni mtu na dada yake wamefariki dunia leo kati ya saa 3:00 na 3:30 asubuhi katika eneo la Pasua Manispaa ya Moshi", amesema Kamanda Issah.

Chanzo - Nipashe
Share:

CUF UPANDE WA MAALIM SEIF WAMUANGUKIA JAJI MKUU

Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa katibu mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kimemuomba Jaji Mkuu na Jaji kiongozi kusaidia kusomwa hukumu katika shauri linalohusu uhalali wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba. Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam  na Mnadhimu wa Kambi ya CUF Bungeni ambaye pia ni mbunge wa Malindi Ally Saleh wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema shauri hilo lililopo mbele ya Jaji Dr.Benhajj Massoud tayari limeshasikilizwa kwa pande zote mbili na lipo katika hatua ya kutolewa hukumu. Mnadhimu huyo amesema kuwa kucheleweshwa kutolewa kwa hukumu hiyo kumeathiri…

Source

Share:

MBUNGE WA CCM AFUNGUKA BAADA YA NDOA YAKE KUVUNJIKA


Mbunge Bonnah Kaluwa

Mbunge wa Segerea (CCM) jijini Dar es Salaam aliyekuwa akitumia jina la Bonnah Kaluwa amekiri kuachana na mume wake Moses Kaluwa na hivyo kulazimika kubadili majina yake ya mwisho.

Mbunge huyo wa CCM ambaye katika mitandao yake ilikuwa ikifahamika kwa jina la Bonnah Kaluwa sasa yanasomeka kama 'Bonnah Kamoli'.

Hata hivyo baada ya tetesi hizo kusambaa kwa kasi, kupitia gazeti linalotoka kila siku Bonna amekiri ukweli wa taarifa hizo.

“Taarifa ni za kweli tumeachana. Ni matatizo ya kifamilia. Nimeshaweka majina yangu kwenye mitandao ya kijamii. Nimeweka Instagram, Facebook. Bunge wana taratibu zao, si wamepata barua", amesema Bona.

Hata hivyo tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado imeendelea kutumia majina yake ya awali ya ‘Bonnah Moses Kaluwa'.
Chanzo - EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger