Wednesday, 16 January 2019

CHADEMA YATUMA SALAMU ZA POLE NCHINI KENYA KUFUATIA SHAMBULIZI LILILOFANYWA JANA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA)kupitia kwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Tumaini Makene kimetuma Salamu za pole kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta na wananchi kwa ujumla kufuatia shambulio lililotokea jana january 15 na watu 14 kufariki. Taarifa iliyotolewa leo kwa waandishi wa habari imesema,CHADEMA imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tukio la shambulizi linalohusishwa na ugaidi, lililofanyika kwenye eneo lenye shughuli mbalimbali za kijamii, katika Hoteli ya DusitD2, Nairobi, nchini Kenya, siku ya Jumanne, Januari 15, mwaka huu. “Kipekee CHADEMA inatuma salaam za pole kwa watu wote…

Source

Share:

MWANAFUNZI ALIYEBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MWENZIE AKANA MAELEZO YA AWALI.

Na,Naomi Milton Serengeti Mathayo Songalaeli (21) mkazi wa kijiji cha Natambiso Wilaya ya Serengeti, amekana maelezo ya awali mara baada ya kusomewa maelezo hayo katika kesi yake ya Jinai namba 94/2018. Kabla ya kusomewa maelezo ya awali Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile alimtaka mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela kumkumbusha mshitakiwa mashtaka yake. Akisoma mashtaka Faru alisema makosa yanayomkabili mshitakiwa ni mawili kosa la kwanza ni kubaka kinyume na kifungu 130(1)(2)(e) na 131(1)cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 Kosa la pili ni…

Source

Share:

Picha:SHIRIKA LA REDESO LAONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI WILAYA YA KISHAPU


Katika mapambano dhidi ya athari zitokananazo na ukataji miti kiholela ikiwa ni pamoja na hali ya ukame mkoani Shinyanga Shirika lisilokuwa la kiserikali la REDESO linalotekeleza mradi wa kukabiliana athari za maafa katika wilaya ya Kishapu limepanda miti zaidi ya 4000 katika kata ya kiloleli kwa lengo la kukabiliana na hali hiyo
 Akiongea na wadau wa mazingira Jumamosi Januari 13,2019 kutoka kata ya Kiloleli, Meneja miradi wa shirika la REDESO Charles Bulegeya amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanachangiwa na shughuli za kibinaadamu ikiwemo kukata miti hovyo.

Bulegeya amesema  wanaendelea kutoa elimu ya madhara ya ukataji miti ili kuiniusuru Wilaya ya Kishapu na hali  ukame  hivyo kwa  kushirikiana na jamii shirika hilo limepanda miti elfu 4000 katika kijiji cha Kiloleli .

“Tumeshirikisha wadau kila kitongoji ili kushiriki zoezi hili la upandaji miti kwenye vyanzo vya maji,maana chanzo hiki cha maji kiloleli kinakabiriwa na kujaa tope kwa hiyo kwa kupanda miti maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji itapunguza upoteaji wa maji” ,alisema Bulegeya 

“Tumepanda miti zaidi ya 4000 katika kijiji hiki cha Kiloleli kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambao walichangangia miti 2000 pia ushirikiano wa mgodi wa mwadui walichangia miti 1000 na taasisi ilipokea miti 1000 kutoka kwa wadau” aliongeza Bulegeya. 

Kwa upande wake kaimu afisa mali asili wilaya ya Kishapu Wilson Bigirwa amesema kuwa Halmashauri hiyo imepanga utaratibu wa kila kaya ihakikishe imepanda miti kumi katika maeneo yao na kuitunza huku akiweka wazi kuwa kufikia mwezi wanne wanatarajia kumaliza zoezi la upandaji miti Wilaya nzima ya Kishapu. 

“Ndugu zangu kwa wale wote tulioshiriki katika kupanda miti tuwe walinzi wa miti yetu itapendeza kabisa kama miti yote tuliyoipanda itakuwa na kuwa mfano kwa watu wengine, na Serikali za kijiji zitunge sheria ndogondogo kuwabana wale ambao hawatakuwa sambamba na sisi”alisema Bigirwa 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kiloleli wamelipongeza shirika la REDESO kwa kutekeleza mradi wa upandaji miti katika Kata yao ili kukabilianan na ukame unaochangia kukosekana kwa maji na kudai kuwa wapo tayari kuwa mabalozi katika utunzaji mazingira kwa kupanda miti . 

Shirika la REDESO linatekeleza miradi mbalimbali katika mkoa wa Shinyanga ikiwa ni pamoja na kuwezesha akina mama na vijana, ubunifu na uboreshaji wa mnyororo wa thamani wa zao la Mkonge kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi na mradi wa tatu ni mradi wa kukabilianaa na athari za maafa.

Meneja miradi wa shirika la REDESO Charles Bulegeya akielezea juu ya umuhimu wa upandaji miti ili kukabiliana na hali ya ukame wilayani Kishapu huku akiweka wazi kuwa shirika la REDESO linatekeleza mradi kukabiliana athari za maafa katika Wilaya ya Kishapu. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog
Kaimu afisa Mali Asili Wilaya ya Kishapu Wilson Bigirwa akiwaelekeza wananchi  namna bora kupanda miti .
 wananchi wa  Kijiji cha Kiloleli wakishirikiana katika zoezi la upandaji miti 


 Mtathimini na mfuatiliaji wa mradi wa kupunguza athari za maafa Isack Jonas (kulia) akishirikiana na moja ya mwananchi wa Kata ya Kiloleli katika zoezi la upandaji miti ili kukabiliana na hali ya ukame katika wilaya ya Kishapu.
 Afisa mradi wa kupunguza athari za maafa Vera Cleophas (kulia) akishiriki katika upandaji miti.

 Baadhi ya wadau walioshiriki katika upandaji miti katika kata ya Kiloleli 




Share:

CHINA YAOTESHA PAMBA MWEZINI

Mbegu ambazo zimepelekwa mwezini na chombo cha utafiti wa anga za juu cha Chang'e-4 zimechipua, mamlaka jijini Beijing zimethibitisha.
Hii ni mara ya kwanza kwa mmea wa kibaolojia kuchipuwa mwezini, na ni hatua inayofungua njia ya tafiti zaidi za kisayansi mwezini.

Chang'e 4 pia ndio chombo cha kwanza kutafiti sehemu ya mbali zaidi ya mwezi, ambayo haitazamani na uso wa dunia.

Chombo hicho kilitua mwezini Januari 3 kikiwa kimebeba vifaa vya kuchunguza jiolojia ya eneo hilo.

Mimea imekuwa ikioteshwa kwenye kituo cha kimataifa cha anga za juu lakini haijawahi kujaribiwa mwezini.

Hii inafungua milango ya uwezekano wa wanaanga kuweza kuzalisha chakula chao wenyewe wakiwa anga za mbali na kupunguza uhitaji wa kurudi duniani ili kufuata chakula.

Chanzo:Bbc
Share:

SANAMU LA SHETANI LASHUTUMIWA KUFURAHI SANA

Sanamu la shetani linalopangwa kuwekwa katika mji wa Uhispania Segovia limeshutumiwa kwa kufurahi sana.

Sanamu hilo la shaba bronze liliundwa kwa heshima ya ngano au hadithi ya kale inayosema kuwa shetani alihadaiwa kujenga bomba mashuhuri la maji mjini humo.

Lakini wakaazi wanasema shetani huyo - anayetabasamu na anayeonekana kupiga slefie na simu ya mkononi - anaonekana kuwa na upole na urafiki mwingi.

Msanii huyo ameiambia BBC ameshangazwa na kiwango cha shutuma zilizoelekezwa kwa kazi yake.

Jaji mmoja sasa ameagiza sanamu hilo lisiwekwe kwa sasa wakati anaposhauriana kufahamu iwapo linadhalilisha Wakristo.

Chanzo:Bbc


Share:

RAIS KENYATTA : MAGAIDI WALIOUA RAIA 14 NA KUJERUHI 30, WOTE WAMEUAWA


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema magaidi wote waliofanya shambulio katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 na kusababisha vifo vya watu 14, wameuawa.

Kenyatta ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 16, 2019 wakati akihutubia Taifa kuhusu operesheni ya kupambana na magaidi waliovamia hoteli hiyo. Tukio hilo lililotokea jana Januari 15, 2019.

Amebainisha kuwa watu 700 wameokolewa na vyombo vya ulinzi na usalama, kwamba operesheni hiyo imekamilika na magaidi wote wameuawa.

Rais Kenyatta amesema watu 30 waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali mbalimbali za mjini Nairobi.

Share:

DOCUMENTARY YA MAONYESHO YA UTALII WA NDANI - 'UWANDAE EXPRO 2019' YAZINDULIWA DAR


Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) akiongea na wandishi wa habari ( hawapo pichani ) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019.

 ” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania” Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TTB ,Geofrey Tengeneza na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko.

Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ,Geofrey Tengeneza (katikati) na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko, wakiwa wameshikana mikono kuonyesha ushirikiano wao kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019.” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania.
---
Chama cha Wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ, wameandaa documentary ambayo imeziduliwa leo jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi wa documentary hiyo ambayo inahusu tukio la maonyesho maonesho ya Utalii wa ndani UWANDAE EXPO 2019 yatakayofanyika mwezi ujao mwezi wa Februari tarehe 15 hadi 17 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa (National Museum –Posta). ilifanyika katika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na waandishi wa habari.

Akiongea kuhusu maonyesho haya ambayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza, Mwenyekiti wa AWOTTA, ambayo inaratibu maonyesho hayo, Mary Kalikawe, alisema AWOTTA na washirika wake waamua kutekeleza mpango mkakati wa Bodi ya Utalii wa kuutangaza utalii wa ndani kwa vitendo kupitia UWANDAE EXPO 2019 na kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Tambua ushindani wa Kibiashara katika Utalii wa Ndani Tanzania”.

“Kuzindua kwa documentary hii ikisisitiza mchango wa akina mama “Nani kama mama” kunaenda sambamba na kuzindua matangazo kwa umma wa Tanzania juu ya uwepo wa sekta kubwa ya utalii humu nchini ambayo ni muhimu ikatambuliwa kusudi ihudumiwe na kupewa umuhimu wake. Sekta hii inachochea uwekezaji kwa wingi kama tunavyoona mahoteli, usafirishaji tangu wa ndege hadi wa bodaboda, biashara ya chakula kila pembe ya nchi, burudani na utalii wa aina nyingine nyingi. Sambamba na uwekezaji huu, sekta ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira kwa wakubwa na wadogo pia inabeba uwezo mkubwa wa kutengeneza kipato kwa mtu mmoja mmoja, makundi na kuchangia kipato cha taifa kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa utalii wa mbuga za wanyama unachangia asilimia 17 ya pato zima la taifa ambayo ni takribani dola Bilioni 2.1 au shillingi zaidi ya trillion 4.7 kila mwaka”. alisema Kalikawe.

Maonesho haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mhe. Dr. Hamisi Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii siku ya Ijumaa tarehe, 15 Februari 2019.

Lengo la Maonyesho haya ni kuanzisha utambuaji wa mapana ya sekta ya Utalii wa ndani na fursa kubwa za uwekezaji na ajira zinazoambatana na kukua kwa sekta hii muhimu. Maonyesho yatawaunganisha wafanyabiashara wa bidhaa na huduma katika maeneo mbali mbali yanayosababisaha safari za watanzania. Wafanya biashara hawa na vyombo vinavyowezesha uwekezaji, watatumia jukwaa hili kukuza uhusiano baina ya washiriki na Watembeleaji wa maonesho. Watu elfu tatu wanategemewa kuhudhuria maonyesho.

Taarifa ya tovuti http://bit.ly/2FDzXer inaonesha takwimu zifuatazo: Kuwa mwaka 2014 jumla ya vitengo rasmi vya chakula vinywaji na malazi wakati huo Tanzania bara vilikuwa 11,136. Kati ya hivi asilimia 51.7 vilikuwa vya chakula na vinywaji wakati asilimia 48.3 vilikuwa ni sehemu za watu kulala.

Kwa upande wa sanaa na burudani, jumla ya vitengo rasmi katika utafiti wa mwaka 2014/15 vilikuwa 239 ambayo ni chini ya asilimia 1 ya vitengo vyote vya biashara vilivyotambuliwa mwaka huo. Kati ya hivi ubunifu na burudani vilikuwa asilimia 35.6, michezo na starehe vilikuwa asilimia 24.3, michezo ya kubahatisha na kubeti ilikuwa asilimia 23.8 na vitengo vya library, kujisomea, makumbusho na burudani za utamaduni ilikuwa asilimia 16.3

Waandaaji wa maonesho wanapenda kutangaza kuwa kupitia uelewa wa upana wa sekta zilizomo katika utalii wa ndani, takwimu hizo hapo juu zimekwishaanza kubadilika na kupanda na mwamko wa watanzania na watoa huduma katika kuboresha utalii wa ndani utapandisha sana ukuaji wa vitengo hivi vya biashara.

Ni muhimu mikoa yote itambue umuhimu wa kuvuta wageni wa ndani kwenda kutembea kwa sababu mbali mbali katika mikoa yao. Kuwasili kwa wageni ndio ukuaji wa sekta ya utalii wa ndani. Takwimu hizo hapo juu zitajidhihirisha katika mikoa mbali mbali ikifanya bidii kuvuta wageni wa ndani na kuwapa huduma nzuri kama vile wanataka wageni wasahau kurudi kwao!

Faida ya kushiriki:

-Kuonyesha bidhaa au huduma wanazozalisha au wanazotoa;

-Kupata fursa ya kujifunza teknonolija mpya na ujuzi kutoka kwa washirikiwengine;

-Kupata fursa ya kushiriki katika kongamano na semina ya bure itakayofanyika sambamba na maonyesho hayo;

-Kukutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji, washauri wa kibiashara na Wasambazaji wa huduma mbalimbali;

-Kupata kutangazwa kwenye utandawazi wa kitaifa na kimataifa kwa njia mbalimbali;

-Kupata fursa mbali mbali ambazo ni pamoja na tiketi ya raffle, vocha ya malazi, zawadi za kusafiri n.k.

Aidha, ni fursa ya kimkakati ya kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kupenda kutumia huduma zinazotolewa na wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.

Maonyesho haya yanatarajiwa kushirikisha, Wizara, Taasisi, Makampuni pamoja na Wafanyabiashara wa sekta mbalimbali. Kongamano litakuwa juu ya "Biashara, Uwekezaji na Ajira katika Utalii wa Ndani ambalo litatolewa bure (idadi ni watu 250 tu kwa siku moja wataruhusiwa, hivyo jiandikishe mapema kabla nafasi hazijaisha).

Kiingilio kwenye maonesho ni bure asubuhi hadi saa 10 jioni. Kisha yanafuata masaa ya burudani ambayo inalipiwa kiasi kidogo.
Share:

HILI NDIO KUNDI LILILOTHIBITISHA KUFANYA SHAMBULIZI RIVERSIDE NAIROBI

Kundi la wapiganaji la al-shabab linakabiliana na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Somalia na limefanya misururu ya mshambulizi katika eneo zima.
Kundi hilo linalohusishwa na al-Qaeda limefurushwa katika miji mingi lililodhibiti lakini linasalia kuwa hatari.

Neno al-Shabab linamaanisha vijana kwa lugha ya kiarabu.

Lilijitokeza kutokana na kundi lenye ititakadi kali la Muungano wa mahakama za kiislamu nchini Somali ambalo lilikuwa likidhibiti mji wa Mogadishu 2006, kabla ya kufurushwa na vikosi vya Ethiopia.

Kuna ripoti kadhaa za wapiganaji wa Jihad wa kigeni wanaoelekea Somalia kusaidia al-Shabab, kutoka mataifa jirani pamoja na Marekani na Ulaya.

Limepigwa marufuku kama kundi la kigaidi na Marekani pamoja na Uingereza na linaaminika kuwa na kati ya wapiganaji 7000 na 9000.

Al-Shabab linahubiri Uislamu wa madhahabu ya Wahhabi kutoka Saudia huku raia wengi wa Somali wakiwa wa madhahabu ya Sufi.

Limeweka sheria kali za Kiislamu katika maeneo linayodhibiti , ikiwemo kumpiga mawe hadi kufa mwanamke anayetuhumiwa kuzini mbali na kuwakata mikono wezi.

Chanzo:Bbc
Share:

TFF KUBURUZWA MAHAKAMANI SHINYANGA SAKATA LA UCHAGUZI WA VIONGOZI YANGA

Mwanachama wa Yanga Chibura Makorongo mkazi wa wilaya na mkoa wa Shinyanga mwenye kadi ya uanachama wa Yanga namba 0015249 amehitaji ufafanuzi kutoka kwa kamati ya shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) inayosimamia uchaguzi wa viongozi wa Yanga, kuhusu tafsiri ya uhalali wa uanachama wa Yanga kupitia Benki ya Posta, pia suala la viongozi wa klabu hiyo kuikacha mikoa mingine kuomba kura za kuiongoza klabu hiyo. 

Chibura amesema hayo wakati akizungumza na www.malunde.com kuhusu sintofahamu ya mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa klabu ya Yanga na kusema kuwa endapo mambo hayo hayatatolewa ufafanuzi yupo tayari kwenda mahakamani kusitisha zoezi la uchaguzi ambalo linasimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF). 

“Wanachama wa Yanga waliopitia mfumo wa kujiunga kupitia Benki ya Posta ni wanachama halali au la! Na kama ni la! Ni nani aliyepitisha suala hilo?” Aliuliza Chibura. 

“Na hao viongozi wanaowania nafasi mbona wameitenga mikoa mingine? Wakipata dhamana ya uongozi watakuwa wanawaongoza wanachama wa Dar es salaam ama wanachama wa nchi nzima? Tunapokwenda kwenye uchaguzi tutakwenda mahakamani hasa mimi nimeshaanza kuwasiliana na mwanasheria wangu,” Aliongeza Chibura.

Klabu ya Yanga licha ya kukabiliwa na misukosuko ya makundi mawili yanayosigana lakini klabu hiyo inakalia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 53,ikiwa imecheza mechi 19 bila ya kupoteza mchezo hata mmoja,ikifuatiwa na timu ya Azam fc yenye alama 40 baada ya kucheza michezo 17,huku Simba Sc ikishikilia nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 baada ya kuchez mechi 14.


Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Share:

Picha : MIGODI YA BUZWAGI , BULYANHULU YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA SHULE KAHAMA


Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imetoa msaada wa mabati 2347 yenye thamani ya shilingi milioni 70 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu katika shule za msingi na sekondari kwenye halmashauri za wilaya ya Msalala na Kahama Mji mkoani Shinyanga. 

Mabati hayo yenye geji 28  yamekabidhiwa leo Januari 16,2019 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha Meneja Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akimwakilisha Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mgongo alisema Acacia inaunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendelo ya Taifa ya mwaka 2025. 

"Katika muitikio wa ombi la msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya madarasa na nyumba za walimu,migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu imechangia vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 150,mpaka sasa tumechangia mifuko ya saruji 3200 ambapo halmashauri ya Kahama Mji imepokea mifuko 1600 ya saruji na Msalala mifuko 1600 jumla ina thamani ya shilingi milioni 80",alieleza Mgongo.  

"Kiasi cha ziada ya fedha iliyobaki ambacho ni sh. Milioni 70 kimetumika kununua mabati haya 2347 yaani mabati 1173 kwa Halmashauri ya Kahama Mji na mabati 1174 Msalala",aliongeza Mgongo. 

Alisema msaada huo utasaidia kuongeza miundo mbinu katika shule ili kukidhi ongezeko la wanafunzi kwani tangu serikali ianze utekelezaji wa mpango wa kutoa elimu bure,uandikishaji wa wanafunzi shuleni umeongezeka na uhitaji wa miundombinu umeongezeka. 

Mgongo alielezea kuwa, kupitia mpango wake wa maendeleo ya jamii,Acacia imeendelea kuboresha upatikanaji wa elimu katika jamii zinazozunguka migodi yake na kuleta mapinduzi ya kijamii na kiuchumi nchini sambamba na ajenda kuu ya viwanda. 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama, Anamringi Macha aliishukuru Acacia kwa kuwa sehemu ya jamii kuchangia sekta ya elimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Macha alisema wilaya yake ina uhitaji wa madarasa 250 na kubainisha kuwa mabati yaliyotolewa na Acacia yatatumika kwenye ujenzi wa madarasa 50 huku akitaja kipaumbele ni kwenye shule ambazo tayari wazazi wamejenga maboma. 

Aidha aliwataka wadau kushirikiana na serikali kuchangia kwenye elimu kwani kila mmoja ni sehemu ya jamii hivyo anatakiwa kuchangia badala ya kuiachia serikali pekee.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mwendeshaji mgodi wa Buzwagi, Arthur Mgongo akizungumza kwa niaba ya Meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakati akikabidhi mabati  2347 yaliyotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Ushetu leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Mgongo akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha (kulia) wakati akikabidhi mabati  2347 (pichani nyuma) yaliyotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kahama Mji na Ushetu. Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija.
Mgongo akielezea shughuli zinazofanywa na Acacia katika jamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maktaba mjini Kahama,Nyang'hwale na Tarime lakini pia maboresho na utanuzi wa shule za msingi na sekondari ikiwemo ujenzi wa maabara na mabweni.
Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji, Underson Msumba akiangalia mabati matatu kati ya 2347 ambapo 1173 ni kwa ajili ya Kahama Mji yaliyotolewa na migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akizungumza wakati akipokea mabati yaliyotolewa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akiishukuru Acacia kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wilayani Kahama kwa kuchangia shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kahama Mji, Abel Shija akielezea jinsi Acacia wanavyoshirikiana na halmashauri hiyo kuwaletea maendeleo wananchi.
Katibu wa CCM wilaya ya Kahama (kwanza kushoto) akizungumza wakati wa makabidhiano ya mabati ambapo alisema mchango wa Acacia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Viongozi mbalimbali wa halmashauri  ya wilaya ya Kahama Mji na Msalala na waandishi wa habari wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya mabati.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

CCM YAUNGA MKONO SHERIA MPYA YA VYAMA VYA SIASA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema sheria vya vyama vya siasa iliyopo sasa haimpi nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi kwa ufanisi hivyo mabadiliko ya muswada mpya yatasaidia uimara wa vyama vya siasa na Ofisi ya Msajili kufanya kazi kwa ufanisi.

Polepole ameyasema hayo leo Jumatano Januari 16 katika mkutano wa chama hicho wa kujadili mabadiliko ya muswada kabla ya kupelekwa Bungeni uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Mabadiliko hayo yatampa nguvu msajili wa vyama vya siasa kutazama kwa jicho la upole endapo chama kimefanya vizuri na jicho la ukali kwa mambo ya ovyo ambayo chama kitafanya,” amesema.

Aidha, amesema mabadiliko hayo yatampa nguvu Msajili kuhusika kwenye usajili wa vyama vya siasa, kusimamia chaguzi za vyama vya ndani, kutoa na kufuatilia uwajibikaji wa ruzuku.

“Sheria tunayoitumia sasa ni sheria ya mwaka 2010 ni miaka 10 imepita tangu kufanya mabadiliko ya sheria, sisi ni vijana tunatakiwa tutoe maoni na mabadiliko ya sheria mpya ili sheria mpya itakayokuja kutumika isiweze kumbana msajili wa vyama vya siasa pamoja na sisi wanachama,” amesema Polepole.


Awali katibu wa siasa na mahusiano ya kimataifa wa CCM, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amewataka wanachana wa chama hicho kutoa maoni yao bila wasiwasi kuhusu muswada huo.

Amesema kusudi kubwa la muswada huo ni kutengeneza mazingira ya kuwaongoza Watanzania kulingana na mazingira yaliyopo.

Amesema muswada huo unapiga marufuku kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi na usalama ndani ya vyama vya siasa jambo ambalo ni sahihi
Share:

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUHUSU UCHAGUZI WA YANGA

Ndugu Wana-habari, Ijumaa iliyopita niliwatangazia kusogezwa mbele kwa muda uchaguzi mdogo wa klabu ya Yanga kufuatia taarifa za wimbi la (tulioamini kuwa wana-Yanga) kufungua kesi sehemu mbalimbali nchini kuzuia uchaguzi huo usifanyike na kwamba baadhi ya Mahakama zilishatoa amri hiyo. 

Kwa kuheshimu mamlaka ya ki-Katiba ya Mahakama nchini na kwamba nchi yetu inaheshimu na kufuata utawala wa sheria, Kamati yangu ya Uchaguzi haikuwa na njia nyingine ya kufanya bali kuusogeza mbele kwa muda uchaguzi wa Klabu ya Yanga uliopangwa ufanyike siku mbili baadaye, yaani Jumapili ya tarehe 13/01/2018. 

Kwa upande wa pili, Kamati ilijikuta na deni kubwa kwa wana-Yanga, deni la kuelezea kilichojiri, kuelezea msingi wa kesi hizo mahakamani zilizosababisha kusogezwa mbele kwa muda uchaguzi katika klabu yao. 

Hivyo kuanzia Ijumaa jioni, yaani mara tu baada ya kutangaza kusogezwa mbele kwa muda kwa uchaguzi huo, Kamati ilitumia njia mbalimbali kuwafikia wale wote waliofungua kesi ili kujua msingi wa malalamiko yao na uhalali wao kusimama mahakamani dhidi ya Klabu hiyo ya Yanga kwa mujibu wa Katiba ya Yanga. 

Tumejiridhisha kuwa malalamiko yote yamejikita kwenye maeneo makuu matatu: (i) mosi, uhalali wa wanachama wenye kadi za zamani, kadi za CRDB na kadi za Benki ya Posta kupiga kura; (ii) pili, kukataliwa majina ya wanachama katika baadhi ya matawi ya Yanga kuingizwa kwenye rejista ya wanachama wa Yanga; na (iii) tatu, sintofahamu ya nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga hivyo kusababisha baadhi ya wanachama wenye sifa za uongozi, kuwa na mashaka kujitokeza. 

Kamati ya Uchaguzi, mbali na kuchambua sifa ya uanachama ya walalamikaji hao (ambapo Kamati imebaini kuwa walalamikaji wote kasoro mmoja, si wanachama hai wa Yanga), imepitia malalamiko yote hayo kwa kina na kuwapelekea ujumbe ufuatao walalamikaji wote kwamba: (i) uanachama wao Yanga una hitilafu ki-Katiba, hivyo hawakuwa na sifa (locus) kupeleka malamamiko yao popote pale kwa kivuli cha uanachama wa klabu hiyo; (ii) Katiba za Yanga, TFF, CAF na FIFA haziruhusu wanachama wao kupeleka malalamiko mahakamani, hivyo utaratibu huo hauna tija mbali na kuiondolea klabu sifa ya kuheshimu taratibu (compliance); (iii) malalamiko yao yote waliyoainisha yanatatulika kwa taratibu zilizopo ndani ya shirikisho, hivyo hawana budi kuondoa kesi hizo mahakamani mara moja. 

Napenda kuwataarifu kuwa walalamikaji wote wametuelewa na wamekubali kuondoa kesi zao zote mahakamami na hivyo, kuruhusu Kamati yangu kuwasilisha TFF malalamiko yote tuliyoainisha ili yafanyiwe kazi ndani ya siku 7 kuanzia jana na baada ya hapo Kamati itatangaza ratiba ya kukamilisha uchaguzi mdogo wa Yanga. 

Naomba vilevile nisisitize kwamba uchaguzi huu ni uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi. 

Hivyo viongozi wa Yanga tunaowachagua sasa ni wa kipindi kifupi kilichobaki cha takriban mwaka mmoja, kabla ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Yanga kuanza. 

Nihitimishe taarifa yangu kwa kuwashukuru Watanzania na wana-Yanga wote kwa utulivu na uvumilivu mkubwa mliouonesha baada ya uchaguzi wenu mdogo kusogezwa mbele kwa muda. 

Aidha nawaomba wana-Yanga wote wakiongozwa na Wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Sekreterieti na Wajumbe waliobaki wa Kamati ya Utendaji, wasichoke maana tumekaribia mwisho wa zoezi hili lenye afya kwa ustawi na maendeleo ya klabu hii kongwe Afrika ya Mashariki na Kati. Timu bora inategemea uongozi bora unaowajibika kwa wanachama. 

AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA
Malangwe Ally Mchungahela
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TFF
Share:

LUGOLA AUNDA KAMATI YA KUCHUNGA MALALAMIKO YA RUSHWA KWA POLISI WA USALAMA BARABARANI

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo aunde kamati ya kuchunguza vitendo na mianya ya rushwa kwa jeshi la polisi na msisitizo mkubwa kwenye kitengo cha usalama wa barabarani.

Akizungumza leo Jumatano Januari 16 2019, Lugola pia amemtaka kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani kujitafakari, kujipima kama anatosha katika nafasi hiyo.


"Nimemwelekeza katibu mkuu aunde timu ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo na mianya ya rushwa na msisitizo mkubwa kwenye usalama wa barabarani na tume hiyo itanipa hatua za kuchukua," amesema.


Amesema kumekuwa na malalamiko mengi yanayohusu ubambikiaji wa makosa ya barabarani kwa madhumuni ya kutaka rushwa na unyanyasaji wa madereva bodaboda.


Ameongeza kwamba licha ya kuwapo makamanda wa trafiki wa mikoa lakini bado kumekuwa na malalamiko juu ya utendaji wa polisi na hivyo ameamua kuchukua hatua dhidi ya vitendo hivyo.


Amesema tume itachunguza kitengo hicho na kumpelekea majibu ili aweze kuchukua hatua.
Share:

WAZIRI MKUU UINGEREZA ASHINDWA KUJITOA UMOJA WA ULAYA 'BREXIT'

Waziri Mkuu wa Uingereza ameshindwa vibaya katika kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya – maarufu kama Brexit – katika bunge la Uingereza baada ya wabunge kupinga mswaada wake kwa kura 432 kwa 202.

Mara baada ya kipigo hicho, May amesema kuwa kutokana na wingi wa kura za kupinga mswaada huo serikali yake itaruhusu mswaada wa kutokuwa na imani kujadiliwa bungeni.

Aidha, wakati anarudi kukaa chini, kiongozi wa chama cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn mara moja alithibitisha kuwa amewasilisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya May, mswaada ambao utajadiliwa Jumatano.


Hata hivyo, May alikuwa amewasilisha mbele ya bunge mpango mzima wa jinsi Uingereza itakavyojitoa katika Umoja wa Ulaya suala ambalo liliidhihirishwa katika kura ya maoni mwaka 2016.
Share:

BUNGE LASITISHA KUFANYA KAZI NA CAG

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad. Aidha Ndugai amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine. Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda. Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni…

Source

Share:

BUNGE LASITISHA KAZI NA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kwa sasa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.
Kutokana na hali hiyo, amewatawanya wajumbe wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Tawala za Mikoa na Mitaa (LAAC) kufanya kazi katika kamati nyingine.

Hatua ya usitishaji huo inatokana na kauli ya Profesa Assad aliyoitoa Desemba mwaka jana katika mahojiano na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Arnold Kayanda.

Mtangazaji huyo alimuuliza CAG kuwa ni vipi ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonesha kuna ubadhirifu, lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.


Katika majibu yake CAG alisema; “Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge".

“Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa",Aliongeza Profesa Assad.

Spika Ndugai jana alisema suala hilo si la utani kama baadhi ya wanasiasa wanavyolichukulia.

Chanzo:Mpekuzi
Share:

WAZIRI MKUU UINGEREZA KUKABILIWA NA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE

Wabunge wa Uingereza Jumanne waliyakataa pakubwa makubaliano ya Waziri Mkuu Theresa May na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo, jambo lililouvuruga mchakato wa Brexit.

Hatua hiyo imepelekea kura isiyokuwa na imani kuwasilishwa, hatua ambayo inaweza kuiangusha serikali ya May. Wabunge walioyapinga makubaliano hayo ni 432 huku walioyaunga mkono wakiwa 202 pekee.

 Kushindwa kwa Waziri Mkuu huyo kulitarajiwa na wengi ingawa kiasi cha kura alizoshindwa nazo ni jambo ambalo limeuharibu uongozi wake unaosuwasuwa.

Kushindwa huku ni kwa kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa serikali kushindwa kwa kiasi kikubwa cha kura katika bunge la Uingereza na kunafuatia msukosuko wa kisiasa wa zaidi ya miaka miwili ambapo May alijiwekea hadhi ya kisiasa kwa kuhakikisha amepata makubaliano ya Brexit. 

Jeremy Corbyn aliwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na serikali ya May

Muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na spika John Bercow Waziri Mkuu May, alizungumza.

Chanzo:Dw
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger