Sunday, 13 January 2019

WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA WADAU WA MRADI WA KUENDELEZA TASNIA YA MBEGU NCHINI

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 12 Januari 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa kuendeleza tasnia ya mbegu nchini.

Katika Kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo I Jijini Dar es salaam pamoja na wadau kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI), na Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), vilevile walialikwa wadau kutoka Bill & Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience.

Akizungumza katika kikao kazi hicho Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuongeza matumizi ya teknolojia ikiwemo mbegu bora.

Alisema pamoja na mambo mengine serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli imjidhartiti katika kuhakikisha kuwa nchi inajitosheleza kwa mafuta ya kula na hivyo serikali inataka mradi huo kuondoa chanagmoto katika sekta ya mbegu kwa kuzalisha mbegu za mafuta hasa za alizeti na michikichi.

Mhe Hasunga amewapongeza wadau kutoka Bill & Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania kutekeleza mradi huo.
Share:

KAULI YA JPM YA 'KUCHINJWA NA KUTUPWA BAHARINI' YAWAIBUA WAPINZANI


Wakati Rais John Magufuli akieleza sababu zinazomzuia kukutana na wanasiasa, viongozi wa vyama vya upinzani wamemtaka asiwe na hofu kukutana nao na kwamba pengine mtu aliyetishia kumchinja, alikuwa na maana ya “kuchinjwa kisiasa”.


Akizungumzia ushauri uliotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la FGBF kutaka wanasiasa wakutane kama walivyofanya viongozi wa kidini, Rais alisema amekuwa akisita kwa sababu baadhi ya wanasiasa wanamtukana na wengine wametishia kumchinja na kumtupa baharini ndio maana ameamua awaache peke yao.

Hata hivyo, alisema yuko tayari kukutana nao.

Hayo yalitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati wa mapokezi ya ndege mpya ya Serikali aina ya Airbus A220-300, ambako viongozi kadhaa wa kidini walipewa nafasi ya kufanya sala, akiwemo Askofu Kakobe, ambaye kabla ya sala aliomba aseme neno.

“Nimeusikia wito wa Mzee Kakobe kuwa walipokutana na wao (viongozi wa dini) kule, basi na sisi wanasiasa tuwe tunakutana,” alisema Rais.

“Mimi nimekubali sana, lakini tatizo ni kuwa huwezi kukutana na mtu anayekutana na kukuambia siku uchinjwe, utupwe baharini. Je, siku ukikutana naye iwe ndiyo siku ya kuchinjwa?”

Kauli hiyo ilimfanya mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda aombe radhi kama kiongozi wa wadau wa siasa na kwa niaba ya vyama vyote iwapo kuna kauli zimewahi kutolewa zenye mbomoko wa maadili.

“Nampongeza kwa kutambulisha utashi wake wa kutaka kukutana na viongozi wa vyama vya siasa. Hivyo kama kuna kauli ambayo imewahi kumkwaza atusamehe sisi wadau wa siasa kama ambavyo amekuwa akisamehe wafungwa ili na sisi tutoke kifungoni. Adhabu ya miaka mitatu inatosha,” alisema.

Alisema Rais anapaswa kuwapangia fursa ya kukutana nao ili awaeleze hisia zake na wao waeleze zao ili kudumisha utamaduni mzuri wa siasa kwa kuwa Tanzania ina deni la kuwa kielelezo cha siasa bora ya demokrasia ya vyama vingi.

Rais hakumtaja mtu aliyetoa tishio hilo la kuchinja, lakini wanasiasa wengi waliotoa lugha iliyotafsiriwa kuwa haifai, wamefikishwa mahakamani na baadhi kama mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi wameshatumikia adhabu ya kifungo.

Naye mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia alisema bado msimamo wake ni meza ya mazungumzo na kwamba hata alipokutana na Rais Ikulu, Novemba 13 mwaka jana alimsisitiza jambo hilo.

“Kauli ya mtu mmoja asiichukulie vibaya. Anatakiwa kujua kuwa yeye ni jalala,” alisema mwenyekiti huyo wa NCCR-Mageuzi akirejea msemo maarufu wa “ukubwa ni jalala”.

“Awe na moyo wa uvumilivu, aweke kipaumbele cha taifa mbele kwa kuwa nchi ni kubwa zaidi ya mtu yeyote.”

Alisema Watanzania wote wanapaswa kutunza nguzo ya hekima, umoja na amani kwa kuwa jamii yoyote yenye migogoro haiwezi kustawi.

Mbatia alitoa mfano wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga ambao siku za hivi karibuni walishikana mikono kumaliza tofauti zao na wamekuwa wakionekana pamoja katika shughuli za kitaifa, kijamii na kiserikali.

Mbatia anaungwa mkono na kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alisema Rais Magufuli hakupaswa kutoa kauli kama hiyo ya “kuchinjwa na kutupwa baharini” kwa kuwa ana cheo cha Rais na amiri jeshi mkuu, lakini akasisitiza kuwa wamekuwa wakiomba kukutana naye kwa mwaka wa pili sasa.

“TCD wamemuandikia barua ya kutaka kuonana naye huu ni mwaka wa pili, lakini majibu yake ndio kama hayo unayoyaona. Hata juzi Mwenyekiti Mbatia alisema kuwa alipokutana naye alimkumbusha,” alisema Zitto

Naye naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salumu Mwalimu alisema kauli ya Rais Magufuli ilikuwa na utata kwa kuwa hakueleza ni kuchinjana kwa namna gani wala ni nani aliyewahi kuahidi kumchinja.

“Kuna vyama vya upinzani 18 yeye hajasema nani anataka kumchinja. Kama kuchinjana kisiasa ni sawa tu kwa kuwa tafsiri yake ni kuchuana, lakini kama ni kuchinjana kwa tafsiri nyingine sio kauli nzuri ina utata ndani yake maana kuchinjana si Utanzania,” alisema Mwalimu.

Kuhusu suala la kukutana na Rais Magufuili, Mwalimu alisema ustaarabu wa siasa ni pamoja na viongozi wa vyama kukutana na kujadili pamoja mambo ya kitaifa, kukosoana kwa heshima na kuruhusu hoja mbadala na hicho ndicho kimekuwa kikifanywa na viongozi waliopita, ndiyo maana siasa za taifa hili zimekuwa zikisifika.

“Siasa zetu zinapaswa kuwa upinzani na ushindani kama ilivyo kwa Simba na Yanga na si uadui. Tukiwa katika majukwaa tunachuana lakini tukishuka chini tunakunywa chai pamoja.

“Tunaoleana na tunashirikishana na kushauriana katika mambo mbalimbali wakati wa tatizo na wakati wa amani. Jambo hilo linarekebisha tabia hata za wafuasi wetu,” alisema Mwalimu.

Alisema Chadema haijawahi kuombwa kukutana na Rais ikakataa, wala haijawahi kusema haitaki kuonana na Rais. Alisema chama hicho kimekuwa kikikutana na marais wote hata Rais aliyepita walikutana naye mara kadhaa kwa kuwa alikuwa na siasa za kistaarabu.

“Hapa nchini kuna Rais mmoja tu, naye ana nafasi ya kutoa mwelekeo wa siasa za nchi. Kama kweli anataka kukutana na viongozi wa siasa ajiamini, aseme wala asiogope.”

Na Ephrahim Bahemu, Mwananchi 
Share:

SHIBUDA : SHERIA HII INAIDHALILISHA CCM....UNAMUOGOPA NANI?


Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa, John Shibuda.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Maswa kupitia CCM, na Maswa Magharibi, John Shibuda amesema Muswada wa Vyama vya Sheria unaotarajia kupelekwa bungeni unaidhalilisha CCM.

Akizungumza jana katika mdahalo wa vyama vya siasa, Shibuda kwa sasa ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi bungeni, amesema CCM kama mzazi wa vyama vingi havipaswi kukandamiza vyama hivyo.

Akifafanua kuhusu kifungu kinachozuia viongozi kuhama vyama na kupewa nafasi za kugombea, Shibuda amehoji kwanini mwanachama azuiwe wakati ni ujuru wake na chama chake kufanya hivyo.

"Unamuogopa nani?, Inamaana ukihama dini moja labda umetoka Uislam kwenda Ukristo usioe mpaka mwaka upite?. Kasema nani? Sheria hii inaidhalilisha CCM. Nawaombeni mnaokwenda kutegeneza sheria mkazijadili kwa kina" Shibuda.

Aidha ameongeza kwamba, "Mzazi wa vyama vingi ni CCM na mlezi wake ni serikali. Sasa mzazi ukizaa mtoto ukamuacha akiwa chokoraa akikutukana usilalamike. Tengenezeni tafsiri ya huu muswada. Chama cha siasa kinapaswa kukonga nyoyo za wananchi na siyo kutegemea kuua chama kingine".
Via>> EATV
Share:

YANGA WATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMUSOKO KUONDOKA YANGA

Uongozi wa klabu ya Yanga umeutolea ufafanuzi ujumbe wa kiungo wake Mzimbambwe, Thaban Kamusoko baada ya kuleta sintofahamu kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kamusoko hivi karibuni aliandika ujumbe huo ukieleza kuwashukuru wapenzi na mashabiki wa Yanga kwa upendo waliomuoneshea tangu ajiunge na timu hiyo.

Kamusoko aliandika ujumbe huo ambapo mashabiki wengi waliokomenti walielewa kuwa ameshaagana na mabosi wake na ikachukuliwa kuwa anaondoka Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari, Dismas Ten, ameibuka na kuutolea ufafanuzi kuwa Kamusoko aliandika na hakuwa na maana ya kuondoka.

Ten ameeleza kuwa ifikie wakati mashabiki wasiwe wanakariri mambo pale mtu anapoandika ujumbe wa aina kama ile, kwani si kweli kuwa anaondoka.

"Si kweli, alichokiandika hakina maana ambayo wengi wametafsiri, bado ana mkataba na Yanga na ataendelea kuwepo" alisema Ten.
Share:

WAZIRI UMMY AWATAKA MADAKTARI KUACHA TABIA ZA KUWA MADALALI WA MADUKA YA DAWA

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaonya madaktari nchini kuacha tabia za kuwa madalali wa maduka ya dawa kwa kuwaandikia wagonjwa dawa mara mbili mbili huku akiwaambia kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali.


Huku akiagiza hospitali za Rufaa kote nchini kuhakikisha zinakuwa na maduka ya dawa litakalokuwa na uhakika wa dawa zote muhimu ili kuondosha kero hiyo na kuondoa mianya ya madaktari kudalalia dawa kwenye maduka binafsi.


Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani wa Tanga aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo na kauli hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walimsimamisha nje ya hospitali hiyo kabla ya kukutana nao.


Wananchi hao ambao walikuwa wakisubiri kuingia hospitalini hapa walimueleza kero hiyo ambapo alisema mbali na kero hiyo aliwaagiza madaktari nchi nzima kuhakikisha wanazingatia mwongozo wa kutoa dawa au matibabu ili kuepusha lawama kwa wagonjwa wa kubadilishiwa dawa na kila daktari.


Akiwa kwenye eneo hilo ambalo ni maalumu kwa ajili ya kupumzikia wananchi ambao wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao kabla ya kuingia hospitalini hapo ndipo wananchi hao walipoamua kumueleza kilio hicho ambacho kimekuwa kikiwaumiza muda mrefu sana na kumuomba akishughulikie.


“Kwa kweli hii sio sawa kabla ya hapa nimepata wasaa wa kuzungumza na wananchi nje ya geti lakini kilio chao kikubwa ni kutokuridishwa na huduma tunazozitoa likiwemo suala la mgonjwa kuandikiwa dawa na kila daktari hii sio sawa naaagiza madaktari acheni kuwa madalali wa maduka ya dawa na sitaki kusikia hili siku nyengine “Alisema Waziri Ummy


Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waziri huyo Mmoja wa wananchi Mussa Jangwa alisema kwamba kwenye hospitali hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ambazo wanakumbana nazo ni kila daktari anayeingia wodini anaandika dawa zake.


Alisema kwamba hatua hiyo imepelekea kuingi gharama kubwa huduma bado ni changamoto kutokana na kutumia fedha nyingi kutokana na kuwepo kuandikiwa dawa kila wakati na kulazimika kwenda kununua


“Mh Waziri tunashukuru kwa kuja na tungeomba viongozi wengine waige mfano wako hapa hospitali ya Bombo kuna tatizo kubwa sana unapo na mgonjwa wodini unapokuja daktari wa kwanza naandika dawa na mwengine akipita anaandika dawa kwenye zamu yake sasa mgonjwa hajui anunue zipo na ghamara zinakwenda “Alisema Mussa.


Alisema wakati wanapoandikiwa dawa hizo wanaelekezwa duka la kwenda kununulia huku wakitumia fedha nyingi ndani ya siku nne jambo ambalo limechangia kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kubaki kuingia gharama zisizokuwa za msingi huku mgonjwa akiwa bado hajatumia akizoandikiwa na hali yake ni mbaya.


“Unapozungumzia jambo la afya ni uhai wa binadahamu nichukue fursa hii kukupongeza kutembelea hospitali hii isiwe ni wewe tu viongozi wote wafanye ziara kama wewe huduma za afya bombo bado changamoto kubwa sana “Alisema


Naye kwa upande wake Pili Nzoya Alisema wakati mwengine daktari anaweza kupita wodini na kumuandikia mgonjwa dawa nyingi wakati ni za kununua na kila wakati wamekuwa wakifanya hivyo na kupelekea kuwepo kwa usumbufu mkubwa kwao.


Awali naye mkazi mwengine Amina Mrisho alimueleza Waziri Ummy kwamba wamekuwa wakiandikiwa dawa wakati bado nyengine walizokuwa nazo hawajazimaliza kitendo ambacho kinawapa wakati mgumu na kujikuta wakiingia hasara.


Alisema kwamba jambo ambalo limekuwa likiwashangaza ni kuandikiwa dawa na daktari halafu wanabadilishiwa dawa nyengine jambo ambalo ni hasara kwao huku wagonjwa wao wakiwa kwenye hali mbaya na baadae mgonjwa anafariki.


“Kwa mfano Mh Waziri umeandikiwa dawa leo za sh.40,000 kabla haujazimaliza unaandikiwa nyengine hili ni tatizo ambalo limekuwa likituumiza sisi wananchi tunaomba utusaidie “Alisema.


Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini walikuwa wanafanya kwa nia njema lakini kama tukiwabaini ambao walikuwa wanafanya kwa nia binafsi tutawachukulia hatua.
Share:

KUSUASUA KWA MIRADI YA MAJI KYERWA NAIBU WAZIRI AAGIZA MKANDARASI KUONDOLEWA

Na mwandishi wetu-Kagera. Kufatia kusuasua kwa miradi ya maji wilayani Kyerwa na kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi wilayani humo,Naibu waziri wa maji Mhe.Jumaa Aweso amemuagiza mhandisi wa maji mkoa wa Kagera kumsimamisha kazi mkandarasi anayetekeleza miradi ya maji wilayani Kyerwa kutokana na kutokuwa na uwezo pamoja na vigezo. Naibu waziri ametoa agizo hilo januari 12 mwaka huu akiwa ziarani katika wilaya za Karagwe na Kyerwa ambapo imeonekena miradi mingi ya maji katika wilaya hizo ni kutokana na makandarasi wanaopewa kazi ya kujenga miradi hiyo kutokuwa na uwezo. Aweso…

Source

Share:

Saturday, 12 January 2019

WASIKIE CCM KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole ameweka wazi mipango ya chama hicho katika kujiandaa na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kumbainisha mgombea kiti cha urais 2020 kupitia chama chao.  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole Polepole kupitia mahojiano yaliyofanyika leo Jan 09 katika kipindi cha East Africa BreakFast amesema kuwa alichokifanya Rais Magufuli kwa kipindi hiki kifupi alichokaa madarakani, ni dhahiri kuwa hakuna mwingine atakayepewa ridhaa na chama zaidi yake kugombea 2020. “Mwaka 2020 hatuna shaka…

Source

Share:

HAIJAWAHI KUTOKEA SIMBA,UKUTA HUU AL AHLY KILIO

Hii ni mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba kwa mabeki wa kati Juuko Murshid na Pascal Wawa kuanza pamoja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. UKUTU wa mabeki wa kati, Pascal Wawa na Juuko Murshid umeonekana kuwa na maelewano mazuri kwenye kikosi cha Simba SC baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura. Ushindi wa mapema wa Simba SC dhidi ya JS Saoura Ndani ya dakika 45 kipindi cha kwanza wa bao 1-0 iliisaidia timu hiyoya Mtaa wa Msimbazi kuja na mipango mizuri…

Source

Share:

SIMBA WAIGONGA JS SAOURA TATU BILA....


Dakika 90 za mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya JS Saoura katika Uwanja wa Taifa zimemalizika wa Simba kuichapa JS Saoura mabao 3 -0.



Dakika ya 45 Okwi alifanikiwa kutumia uwezo wake wa mguu wa kushoto kumalizia pasi ya Clyetous Chama ambaye alipiga pasi mpenyezo iliyomkuta Okwi akawaminya mabeki waarabu na kumalizia kwa shuti kali.

Dakika ya 52 Okwi anamtengenezea pasi Kagere ambaye anaandika bao la pili kwa Simba.

Dakika ya 63 Kagere akamalizia pasi ya Okwi na kuandika bao la tatu kwa Simba Uwanja wa Taifa.

Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Wallace Karia, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na Mfanyabishara Mohamed Dewji walipokuwa wakishangilia goli la tatu la Simba.

Share:

OKWI NOOMA!! ANAIANDIKIA SIMBA BAO LA PILI DAKIKA YA 51


Mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Simba raia wa Uganda, Emmanuel Okwi anafanikiwa kuonyesha thamani yake ya umataifa kwa kufunga mabao maridadi kabisa dakika ya 45 na 51 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura Uwanja wa Taifa.
Matokeo hadi sasa dakika ya 51 ni 2-0
Share:

HAKUNA MJASIRIAMALI MWENYE SIFA ATAKAYEKOSA KITAMBULISHO-DC NJOMBE

Na Amiri kilagalila Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo kiwilaya na kuwahakikishia wote wanao stahili kupata vitambulisho kabla ya mwezi kumalizika. Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe amesema kuwa mala baada ya kusajiliwa na kupata kitambulisho hicho hategemei kuona mjasiriamali yeyote akifanya shughuli zake katika maeneo yasiyokuwa rasmi. “zoezi hili linaendeshwa kwa maagizo ya muheshimiwa Raisi na leo sisi tunazindua sio mwisho lakini hatutalifanya kwa mda mrefu na tunatamani kufika mwisho…

Source

Share:

NHIF YAJIVUNIA UPATIKANAJI WA HUDUMA BORA NCHINI

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umejivunia kuongeza wigo wa wanufaika kwa kuwafikia Wananchi mbalimbali ikiwemo Wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika kwenye huduma ya Ushirika Afya na watoto kupitia huduma ya Toto Afya Kadi. Mfuko pia umewezesha upatikanaji wa huduma za Madaktari Bingwa katika mikoa ya pembezoni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa katika Hospitali hapa nchini. Hayo yameelezwa na Meneja uhusiano wa mfuko huo Bi. Anjela Mziray wakati wa ziara maalum ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya na taasisi zake katika kampeni…

Source

Share:

HIKI NDIYO KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA JS SAOURA

Kikosi cha Simba kitakachocheza leo dhidi ya JS Saoura, mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Share:

KIKWETE,MAGUFULI WAKWAMA KUFIKA SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Rais Mstaafu Kikwetena Rais wa sasa Dkt John Magufuli

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Alli Mohamed Shein ametaja sababu za kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza kwenye hadhara hiyo Rais Shein amesema sababu iliyowafanya Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli, kuwa ni viongozi kupatwa na dharula.

Akizungumzia miaka 55 ya mapinduzi Rais Shein amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itaendelea kulinda usalama wa nchi na kudumisha upendo na amani.

“Ninawahakikishia kuwa nchi yetu iko salama na itaendelea kubaki salama na serikali zetu mbili zitaendelea kutimiza majuku yake ipasavyo na tutahakikisha amani na utulivu vinadumishwa na sheria zote zinafuatwa."

“Mimi na rais Magufuli tutahakikisha Muungano wetu unadumu kwa dhamira ile ile ya viongozi wetu waliopita ili nchi yetu izidi kubaki na amani”, amesema Dkt Shein.
Share:

ALIYETUNGA WIMBO AKIJITANGAZA KUWA NI SHOGA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Share:

SINGIDA UNITED YASAJILI MAKOCHA WAWILI KUTOKA SERBIA

Uongozi wa klabu ya Singida United umeamua kuvunja benki kwa kuwasajili Makocha wawili kutoka Serbia kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo.

Popadic Dragan ambaye ni Kocha Mkuu ameamua kuja na mwenzake ambaye atakuwa Msaidizi, Dusan Momcilovic.

Usajili wa makocha hawa umefanikiwa ikiwa ni baada ya klabu hiyo kutokuwa na Kocha Mkuu tangu kuondoka kwa Hans Van Der Plujim ambaye alitimkia Yanga.

Pengine Singida wameamua kuboresha benchi la ufnudi kwa ajili ya michuano ya SportsPesa Super CUP itakayokuja hivi karibuni.
Share:

KIUNGO WA CHELSEA AJIUNGA MONACO


Kiungo wa klabu ya Chelsea, Cesc Fabregas, amejiunga na klabu ya Monaco, kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 amejiunga na timu hiyo kuungana na nyota mwenzake wa zamani wa klabu ya Arsenal, Thienry Henry, ambaye kwa sasa ndio kocha wa Monaco.

Kiungo huyo tangu awasili Maurizio Sarri, katika klabu ya Chelsea, amekuwa na mgumu sana kupata nafasi tayari msimu huu ameanza michezo sita tu kwenye ligi kuu England.

Fabregas, ameshinda mataji mawili ya ligi kuu England ,na kombe la FA Cup mara mbili.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger