Na Mwandishi wetu Mwanza
Maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yenye kauli mbiu ya “Miaka 50 ya MARPOL, Uwajibikaji wetu unaendelea” yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho tarehe 22 juni,2023 kwenye Viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela, Jijini Mwanza ambapo mgeni rsmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Ujenzi na uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe.Suleiman Masoud Makame
Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za Tasac jijini mwanza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Bw. Nelson Mlali amesema siku ya Mabaharia Duniani huazimishwa wiki ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka Duniani kote na Nchi wanachama wa Shirika la Bahari Duniani(IMO) ambapo Tanzania ni Nchi mwanachama na kwa mwaka huu 2023 maadhimisho haya yatafanyika Kitaifa Jijini MWANZA
Bw. Mlali amesema Maadhimisho haya yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo maonesho ya Taasisi zinazojihusisha na masuala ya usafiri kwa njia ya maji,warsha ya wadau itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa, kufanya usafi katika mialo, kutoa elimu kwa wadau na Wanafunzi wa Vyuo, na zoezi la majaribio ya uokoaji inapotokea dharura majini
“Maonesho haya yatahusisha wadau wote wa Sekta ya Uchukuzi kwa njia ya Maji ambapo watapata fursa ya kutangaza shughuli na majukumu yanayotekelezwa na taasisi zao,kutoa elimu ya uhamasishaji katika shule,vyuo,mialo pamoja na masoko ya samaki yaliyopo jijini mwanza” amesisitiza Mlali
Aidha Bw. Mlali amesema katika siku ya kilele cha maadhimisho tarehe 25 Juni,2023 kunatarajiwa kuwa na mbio za hisani (SeaFarers Marathon) zitakazoanzia katika mwalo wa kirumba kupitia barabara ya isamilo,samaki kutokea nyamagana,kamanga feri na kumalizikia katika mwalo wa kirumba ambapo utafanyika usafi wa mazingira na kugawa Medali kwa washiriki wote na baadae kuelekea katika viwanja vya furahisha kwa ajili ya kufunga maadhimisho
“Natoa rai kwa wananchi wote kutoka sehemu mbalimbali za Viunga vya Jiji la Mwanza na Mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi na kutembelea katika viwanja vya maonesho ili kupata elimu ya usafiri majini na kujiandikisha kwa wingi kwenye mbio za hisani kwani hakuna gharama za uandikishaji na kutatolewa tshirt na medali kwa washiriki wote” ameongeza Mlari
Maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yanayoanza tarehe 22 mpaka 25 Juni, 2023 yanayofanyika kitaifa Jijini Mwanza yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta Uchukuzi kwa Tanzania Bara kupitia Shirika la uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) na Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Zanzibar(ZMA), Pamoja na wadau mbalimbali wa Uchukuzi kwa njia ya maji Nchini.
0 comments:
Post a Comment