Monday, 12 June 2023

HOLYSMILE WAKABIDHI TUZO WADAU SHUPAVU KISHAPU

...



Na Sumai Salum Kishapu

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Holysmile yenye makao yake makuu wilayani Kahama mkoani Shinyanga iliyoanzishwa na kusimamiwa na Bw. Arnold Bweichum imekabidhi tuzo 37 kwa wadau shupavu mbalimbali wilayani Kishapu mkoani humo.


Usiku huo wa tuzo umefanyika Juni 10, 2023 katika ukumbi wa Stage 2 hotel uliopo Mhunze huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Mkude ambapo amesema kuwa mashindano hayo yanaleta chachu yenye lengo la kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya kwa ujumla.


"Vijana hawa wamekuwa wabunifu kwa kuanzisha jambo hili nyeti sio tena vijana wanaokaa mitaani na kulalamika kuwa maisha magumu zaidi sana itawasaidia watu wote watakaopata tuzo hizi kuendelea kuwa na bidii katika utendaji kazi kwa ufanisi zaidi huku wakijua kuna watu wanatambua na kuthamini mchango wao na nipende kuwakaribisha tena Kishapu mwakani kwenye msimu wa pili wa utoaji tuzo za mdau shupavu", amesema Mkude.


Aidha Mkude ameongeza kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali kuwekeza wilayani Kishapu hususani eneo la Maganzo kwa kuwa ni rafiki kwa uwekezaji wowote sanjari na kuwakaribisha kwenye ofisi yake kwa misaada mbalimbali ikiwemo msaada wa kisheria.


Mkurugenzi wa Holysmile Bw. Arnold Bweichum amesema lengo la utoaji tuzo hizo ni kutambua juhudi za wadau na kuchochea huduma chanya kwa jamii, kufungua fursa za uwekezaji wa kibiashara, kuhamasisha na kuhimiza shughuli za kimaendeleo afya na uchumi, kuwatambulisha watu mbalimbali na bidii wazifanyazo pamoja na kuwatambulisha ndani na nje ya maeneo yao mpaka kufikia hatua ya kimataifa kutokana na bidii zao.


"Niwashukuru sana wana Kishapu kwa kuwa shapu kuchangamkia fursa ya tuzo hizi kwa kuwa huu ni msimu wa kwanza Huku hapo kabla nilianzia Wilaya ya Kahama baadaye nikaja Shinyanga mjini na sasa tumeona tuje na Kishapu lengo letu si kuweka chuki naona ya washindani mbalimbali hapana ni kupanua mipaka ya kazi zetu na tujifunze kufanya vizuri zaidi na zaidi", ameongeza Bweichum.


Baadhi ya wadau walioudhuria kwenye sherehe za tuzo hizo wameipongeza Holysmile kwa ubunifu huo na kufikia Kishapu na imewatia moyo na kuwapa mwamko wa kujituma zaidi kwani juhudi zao zinaonekana.


Jumla ya tuzo 5 za heshima zilizotolewa ni pamoja na tuzo kwa DC, DED, halmashauri, Mwenyekiti Halmashauri ya Kishapu na (Mkamba Co.ltd pamoja na Williamson Diamond Co.Ltd) tuzo zingine ni kwa hospitali ya Jakaya Kikwete Kishapu ,RUWASA,REDESO,Kanawa sekondari,Shinyanga sekondari,Kishapu Girls,Mwadui Lutheran Sekondari,Mlimani shule ya msingi, Mkulima Bora wa mkonge(Nkinda Kulwa),mfugaji Bora, mnunuzi Bora wa nafaka,msindikaji Bora wa chakula(Kishapu Food),Kishapu oil, mfanyabiashara Bora (Nasoro Salum),NMB,Kata ya Maganzo,Stage 2 hotel,Milembe lodge, Stom palace bar.


TAARIFA KUTOKA HOLYSMILE

ASANTEEENI KISHAPU, ASANTEEE WADAU SHUPAVU 💪
__________
Tunatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa serikali na WadauShupavu Wilaya ya Kishapu kwa kutupokea kwa Msimu wa kwanza kwa kutupa Ushirikiano. Nichukue Fursa hii adhimu kuwashukuru kwa kuhudhuria katika Hafla ya Usiku wa Wadau Shupavu 2022/23 Kwa Hakika Mmejua kutuheshimisha Mwenyezi Mungu awaongoze kwenye kila Hatua ya Majukumu yenu kwa Hakika Ninyi Ni Wadau Shupavu, Karibuni kwenye msimu Mpya wa 2023/2024

Mh. Joseph Mkude, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu (Mgeni Rasmi) Taasisi inatoa shukrani za dhati kwako kwa kukubali kuitikia mwaliko wetu na kuwa Mgeni Rasmi katika tamasha hili, hii kwetu ni heshima kubwa sana, na hakika Mungu akubariki sana.

Pili, tunaushukuru sana uongozi wa Halmashauri ya Kishapu, hakika wametupa ushirikiano wa 100%, bila wao tusingefanikisha ufanyikaji wa tamasha hili.

Tatu, tunawashukuru sana wadhamini wote waliotuunga mkono kufanikisha tamasha hili, kuwataja wote haitoshi, lakini itoshe kusema tunawashukuru sana, na Mungu awazidishie pale walipopunguza wakawezesha tamasha hili.

Mwisho, tunawashukuru washiriki wote kwa kukubali kushiriki ushidani wa tuzo zao Pamoja na mashabiki wao wamesimama imara kuanzia hatua ya mwanzo ya mapendekezo, upigaji wa kura hadi leo siku ya tamasha wamekuja ukumbini kushuhudia na kutuunga mkono, ni upendo mkubwa sana, kishapu ahsanteni sana, ninyi ni mabingwa na kazi iendelee.
-------------------------------------------------
Tunaomba Radhi Kama Kuna Baadhi ya Changamoto zimejitokeza Kwa Kuwa huu ndio Mwanzo Kwa Kishapu Next tutaboresha Zaidi. Kwa hapa tulipo fanya Ashukuliwe Mungu🙏
Kipekee napenda kuwashukuru wadhamini wetu.
➡️ OFISI YA MKUU WA WILAYA
➡️ HALMASHAURI WILAYA YA KISHAPU
➡️NKAMBA GROUP
➡️TBL
➡️WADAU SHUPAVU WOTE

kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila hatua mmekuwa wadau wa muhimu sana katika kuhakikisha tunafanikisha hafla hii ya usiku wa mdau shupavu Kishapu Msimu wa kwanza
2022\2023 tunaahidi kuendeleza ushirikiano wetu. Ahsanteni sana 🙏💪
___________
Sisi ni HolySmile ✅✅🎖️
https://ift.tt/CSJDu53
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger