Watu 15 wameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine 11 wakijeruhiwa baada ya kuvamiwa na majambazi katika baa moja iliyopo kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo ya habari nchini humo, tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Jumapili, Julai 10, muda mfupi baada ya saa sita usiku.
Watu wengine 11 walijeruhiwa katika kisa hicho ambapo walikimbizwa hospitali huku nane kati yao wakiwa mahututi.
“Ndio, ninaweza kuthibitisha kuwa kisa hicho kilitokea mwendo was aa sita na nusu asubuhi hii,” Kamishna wa Polisi wa Gauteng Elias Mawela amenukuliwa na eNCA, ambalo ni shirika la habari la nchini humo.
Kamishna huyo wa polisi vilevile alisema kuwa waathiriwa ni wa kati ya umri wa miaka 19 na 35. Washukiwa wanaripotiwa kutoroka punde tu baada ya kutekeleza kisa hicho.
“Mwanzo wa upepelezi unaonyesha kuwa watu walikuwa wanaburudika katika eneo moja la burudani. Waliingia na kuwamiminia risasi kiholela,” Mawela alisema.
0 comments:
Post a Comment