Tuesday 12 July 2022

AJALI YAUA WATU NANE, KUJERUHI WATANO BUHARAMULO

...

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, William Mwampaghale

**
Watu nane wakiwamo watano wa familia moja ambao ni mama na watoto wake wanne, wamefariki dunia baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso usiku wa kuamkia Julai 11, 2022, katika eneo la Busiri barabara kuu ya kutoka Lusahunga kuelekea Nyakahura wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera William Mwampaghale, amesema kuwa ajali hiyo imeyahusisha gari la mizigo lililokuwa likitokea nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam, likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda, na Toyota Succeed lililokuwa likitokea eneo la Nyamalagala wilayani Biharamulo kuelekea Benaco wilayani Ngara likiendeshwa na Nyawenda Bihela (35) ambaye alifariki wakati wa ajali hiyo.

"Uchunguzi wa awali umeonesha ajali hiyo imetokana na uzembe wa dereva wa lori kutokana na kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia, kitendo kilichosababisha magari hayo kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo, miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika kituo cha afya Nyakanazi Biharamulo" amesema Kamanda William.

Kamanda huyo amesema kuwa mbali na dereva pia watu wote waliokuwa katika gari aina ya Toyota Succeed walipoteza maisha, na kutaja majina yao kuwa ni Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6), Vedastina Sekanabo (8), Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32).

Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger