Tuesday 26 July 2022

MVUA YAUA WATU 310

...


Takribani watu 310 wamefariki dunia na wengine 300 wamenusurika kifo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko nchini Pakistan.

Mamlaka ya Taifa ya Kusimamia Majanga (NDMA) imetangaza taarifa hiyo na kueleza kwamba wanawake na watoto 175 ni miongoni mwa wahanga wa janga hilo.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa watu 64 wamefariki dunia Mashariki mwa Mkoa wa Punjab, 62 wamefariki Kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Khyber Pakhtunkwa na zaidi ya watu 70 wapoteza maisha Kusini mwa Mkoa wa Sindh.


Aidha, mamlaka hiyo imeongeza kuwa nyumba 8,979 na takribani madaraja 50 yameharibiwa kwa kusombwa na maji ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.


Taarifa inaeleza kuwa Jeshi la wanamaji la Pakistan linaendelea na operesheni za kutoa misaada kwa waathirika wa mafuriko sambamba na kuwahamisha watu wanaoishi kwenye maeneo hatarishi zaidi.


Mamlaka ya hali ya hewa ya Pakistan imetabiri kuwa mvua kali zilizoanza kunyesha Juni 14, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya nchi zitaendelea kunyesha kwa muda wa siku kadhaa nchini humo.


Mnamo 2021 mamia ya watu walifariki dunia na kujeruhiwa ambapo nyumba nyingi zilibomoka kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kali za msimu zilizonyesha katika maeneo mbalimbali ya Pakistan.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger