Friday, 8 July 2022

DIWANI AFARIKI GHAFLA MSIKITINI

...


CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepata pigo kufuatia Diwani wake wa Kata ya Mahohe Mohamed Ngonde, kufariki leo alfajiri.


Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Busoro Pazi, alisema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki akiwa katika Ibada ya alfajiri leo Julai 8, 2022 akiwa ibadani msikitini.


Katibu wa Madiwani Busoro Pazi amesema taratibu za mazishi bado kila wakati atakuwa anatoa taarifa baada kukaa na familia ya marehemu.


"Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana "amesema Busoro.


Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde amesema taarifa za Kifo cha MH, Diwani wake Mohamed Ngonde alifariki na taarifa alitoa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo amesema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki ghafla.


Mwenezi CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde amesema kila wakati taarifa kamili zitatolewa kuhusiana na msiba huo mzito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wana CCM kwa ujumla.


Alhaj Said Sidde,pia ongeza kuwa alimwelezea Mh Ngonde kuwa kada mahiri aliyekitumikia chama cha Mapinduzi kwa muda mrefu na kushikilia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti serikali ya mtaa Kichangani ,Majohe
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger