Kiongozi wa upinzani nchini Malawi Lazarus Chakwera anaelekea kushinda marudio ya Uchaguzi wa urais uliofanyika wiki hii, wakati huu Tume ya Uchaguzi ikitarajiwa kumtangaza mshindi.
Ripoti kwenye vyombo vya Habari na kile cha taifa MBC zinaonesha kuwa Chakwera anaongoza kwa asilimia 60, huku rais anayemaliza muda wake Peter Mutharika akiwa na asilimia 39.
Wafuasi wa bwana Chakwera tayari wameanza kusherehekea kile wanachoamini ni ushindi wa kihistoria baada ya mahakama kufuta uchaguzi wa awali kwa madai ya udanganyifu, na kuitaka Tume ya Uchaguzi kuitisha uchaguzi mwingine wa marudio, na matokeo yake upinzani kuibuka na ushindi ukichukua madaraka kwa njia ya kidemokrasia.
Tume ya Uchaguzi imekuwa ikitoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuwa watulivu, wakati huu ujumuishwaji wa matokeo ukiendelea.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Tume hiyo Chifundo Kachale, amekanusha madai kuwa hakukuwa na waangalizi wa kimataifa wakati wa Uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment