Monday, 25 May 2020

HUYU NDIYE MWANAMKE ANAYEJULIKANA KWA KUPIGWA BUSU MARA NYINGI ZAIDI DUNIANI

...

Wakati flani katika karne ya 19, mwili wa msichana mdogo ambaye alikuwa amekufa maji uliopolewa katika mto Seine.

Kama ulivyokuwa utamaduni wakati huo, mwili wake ulikuwa wazi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha mjini Paris, kukiwa na matumaini kwamba huenda mtu anaweza kuuona na kumtambua, lakini hakuna aliyemtambua.

Katika picha hii ya maelezo iliyopigwa mwaka 1816, watu wanaonekana wakitembelea chumba cha wafu wakitazama miili , kitu kilichopendelewa sana wakati huo.

Daktari wa upasuaji aliyekuwa katika zamu alivutiwa na tabasamu ya uso wa msichana huyo hatua iliomfanya kumuomba mtengenezaji mask au barakoa kuunda uso kama wake.

Ni kutokana na hatua hiyo ndipo sasa uso huo wa mwanamke aliyefariki ulihifadhiwa milele.

Uso kuhifadhiwa
Baadaye, mask hiyo ilianza kuonekana ikiuzwa huku uso huo wa msichana huyo mdogo ukionekana kama unaowapatia msukumo wasanii, washairi na waandishi wa riwaya, wote wakijaribu kubuni hadithi kuhusu mwanamke huyo waliyemtaja kuwa Mona Lisa aliyekufa maji.

Miaka mingi mshairi kutoka Austria na mwandishi wa riwaya Rainer Maria Rilke, raia Mfaransa Louis Aragon, msanii wa Marekani Man Ray na mwandishi wa riwaya wa Urusi Vladimir Nabokov wote walivutiwa na mask hiyo na kuna kipindi fulani hakuna saluni iliyokosa mask hiyo katika ukuta wake Ulaya.

Mojawapo ya hadithi za kwanza ambapo mask hiyo ilionekana ni ile ya riwaya ya 1899 Kwa jina 'The worshiper of the image' iliyoandikwa na Richard le Galliene, ambayo inaelezea jinsi mask hiyo 'inavyomroga' na kumuharibu mshairi mchanga.

Wengi wao wanaelezea hadithi hiyo ya msichana asiye na hatia anayewasili mjini Paris kutoka mashambani , anatongozwa na mtu tajiri na kuachwa anaposhika ujauzito wake . Baada ya kukosa mtu wa kumsaidia , anajirusha katika mto Seine.

Lakini kuna hadithi nyingine.

Ni kufa maji kwa aina nyingine - ama tukio la kufa maji lililosaidia jina la msichana huyo kuingia katika historia ya tiba duniani.

Mwaka 1955 raia wa Norway kwa jina Asmund Laerdal aliokoa maisha ya mwanawe wa kiume , Tore kwa kuuopoa mwili wake katika maji kwa wakati na kuweka wazi njia zake za kupumua mwilini.

Wakati huo, Laerdal alikuwa muundaaji wa wanasesere, kama vile doli na magari kutokana na plastiki laini.

Alipotakiwa kutengeneza kifaa cha kufunza watu mbinu mpya ya kuwafufua inayoshirikisha kumfinya kifua na 'kumpiga busu' hatua inayoweza kuokoa moyo wa mwanadamu ambao ulikuwa umeacha kupiga.

Uzoefu alioupata na mwanawe wa kiume miaka kadhaa iliopita ulimfanya kukubali.

Aliamua kuunda mwanasesere aliyekosa fahamu ambaye alikuwa anahitaji CPR ili kukufuka. Laerdal alimtaka mwanaseser wake kuwa asili.

Na aliona kwamba mwanasesere wa kike hatawaogofya wale watakaokuwa wakifunzwa kufufua mwanadamu CPR (cardiopulmonary resuscitation). Alikumbuka mask iliyokuwa imetundikwa ukutani katika nyumba ya bibi yake, hivyo basi akaamua kwamba uso wa musk hiyo ndiyo utakaotumika katika mafunzo hayo.

Hivyo basi iwapo wewe ni miongoni mwa watu milioni 300 waliofunzwa CPR umefanikiwa kuweka mdomo wako katika mdomo wa mask hiyo ya msichana.

Hio ndiyo sababu anaitwa mwanamke aliyepigwa busu mara nyingi zaidi duniani.

 CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger