Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo wa dola milioni 500 kwa Tanzania, uliopewa jina la mradi wa uboreshaji wa elimu kwa shule za Sekondari (SEQUIP), ambao utanufaisha wanafunzi milioni 6.5, kwa kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kumaliza elimu yao katika mazingira bora.
Akizungumza wakati wa Mkutano huo Mkurugenzi mkaazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Mara Warwick, amesema kuwa hiyo ni hatua muhimu ya kuweza kukabiliana na changamoto za kielimu wanazokumbana nazo watoto.
"Kila mtoto nchini Tanzania anastahili kupata elimu nzuri, lakini maelfu wananyimwa fursa hii ya kubadilisha maisha kila mwaka, mradi huu umetoa kipaumbele zaidi kwa watoto hawa katika kupata haki yao ya msingi ya elimu na kuweka mazingira mazuri kwa watoto wa kike" ameeleza Warwick.
0 comments:
Post a Comment