Friday, 10 January 2020

Profesa Mbarawa Nitazivunja Bodi Za Maji Zitakazoshindwa Kukusanya Mapato Ya Maji

...
SALVATORY NTANDU,SHINYANGA
Waziri wa Maji, Profesa Makama Mbarawa asema ataifuta bodi mpya ya Maji ya Malmlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA)  endapo itashindwa kukusanya mapato kutoa shilingi milioni 691 za sasa hadi kufikia milioni 700.

Uamuzi huo ameutoa jana mjini Shinyanga katika hafla ya kuipitisha bodi hiyo mpya ambayo imeanza kazi rasmi ya usimamizi na uendeshaji wa shughuli za Maji katika Manispaa ya shinyanga kwa kipindi cha miaka 3.

“Kama hamtafikia makusanyo ya mapato ya shilingi milioni 700 ni lazima niivunje bodi hii, muda wa kubembelezana umekwisha bondi nyingi zimekuwa zikifanya kazi kwa mazoea kwa kupeana posho na safari amabazo hazina tija na kushindwa kuzisimamia mamlaka za maji”alisema Profesa Mbarawa.

Kwa mwaka mamlaka hii inakusanya shilingi zaidi ya shilingi bilioni 5.9  lakini makusanyo ya mamlaka hii yako chini ikilinganishwa na Idadi ya watumiaji wa maji ambao ni wengi jambo ambalo linaonesha kuwa katika Mamlaka hii kuna  uzembe katika usanyaji wa mapato na kuisababishia serikali kukosa mapato.

“Mwezi oktoba mwaka jana mmekusanya shilingi milioni 667, septemba 679,  Agosti 691 fedha hizi hazitoshi ikilinganishwa na maji mnayozalisha  ambayo ni lita milioni  438 lakini maji  lita milioni 365 ambapo maji ambayo yanaonekanakupotea njiani ni lita milioni 75  kwa upotevu  lazima bodi hii mpya ianze kuifanyia kazi suala hili” alisema Profesa Mbarawa.

Waziri mbarawa aliongeza kuwa ni lazima mamlaka zote nchini kuhakikisha zinaongeza makusanyo kwa kuanzisha miradi ya mipya ya maji ikiwa ni pamoja na kuongeza matandao wa maji ili kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma za maji karibu na maeneo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Flaviana Kifizi alisema kuwa watahakikisha wanadhibiti upotevu wa maji kwa kushirikiana na Bodi mpya chini ya Mwenyekiti Mwamvua Jirumbi kwa kutekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na serikali ili kuboresha utendaji kazi utakaosaidia kuongezeka kwa mapato.

Amefafanua kuwa SHUWASA inatekeleza miradi ya maji katika wilaya za Kahama kwenda ngogwa hadi kitwana,na Katika wilaya ya Shinyanga ni kutoka Negezi hadi Mwawaza kwa kuwatumia wataalamu wa ndani kupitia Force account ambapo miradi hii imefikia katika  hatua mbalimbali na mafundi wapo katika maeneo ya Miradi.

Nae mwenyekiti aliyemaliza muda wake Deogratius Sulla alisema taasisi za umma zinasuasua kulipa madeni ya Ankara za maji za kila mwezi na kusababisha deni kuendelea kuongezeka hadi kufikia shilingi mlioni 949.

“Mpaka mwezi Disemba mwaka jana JWTZ ilikuwa inadaiwa shilingi milioni 520,244,957,Magereza shilingi milioni 256,520,120,Polisi shilingi 172,346,465”alisema Sulla.

Bodi ambayo imemaliza muda wake ilizinduliwa rasmi Novemba 14 mwaka 2016.

Mwisho.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger