Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri,ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa sehemu ya kuilinda amani ya Tanzania ili kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla na kuendelea kuifanya tanzania kuwa ndio sehemu pekee yenye amani ya uhakika Duniani.
Pamoja na hayo amewakaumbusha wananchi wa mkoa wa Njombe kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani hapo baadaye mwaka huu
Ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Angricana dayosisi ya Tanganyika magharibi lililopo mtaa wa Mji mwema mjini Njombe wakati wa ibada ya mwaka mpya ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kulinda amani.
“Tusichezee amani watanzania wenzangu,kuna watu wachache ambao hawajui amani kwamba ni pamoja na uhai wako,amani hii ambayo ndio msingi wa taifa letu,tusithubutu kuivuruga kwa wakati wowote wala kwasababu yeyote wala kwa ushawishi wa aina yoyote ile”alisema Ruth Msafiri
Aidha ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kujiandikisha na kuhakiki katika daftari la mpiga kura, zoezi lililo anza hii leo na kumalizika januari 5,2020 mkoani humo.
Mchungaji wa kanisa hilo Ayub Haule amesema uwepo wa amani katika taifa hutoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo ni vema kila mtanzania kuwa sehemu ya kulinda amani ya Tanzania
“Tunao uchaguzi mkuu wa nchi hii ambao tunategemea kabisa kama amani ilivyoendelea kudumu ndivyo tutakavyofanya,tunapokuwa tunauona mwaka huu tuone ambavyo tunaweza kupambana na adui mkubwa anayetusakama katika mkoa wetu nae ni maambukizi ya VVU”alisema mchungaji Ayub Haule
Nje ya ibada baadhi ya waumini wamekiri kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilindi amani iliyopo.
Mwaka 2019 umekamilika hapo jana ambapo watanzania waliungana kwa pamoja kuukaribisha mwaka mpya 2020 ambapo walio wengi wamekuwa wakituma maombi yao kwa Mungu ili mwaka huu 2020 uwe mwaka wa mafanikio makubwa katika maisha yao
0 comments:
Post a Comment