Sunday, 25 August 2019

WAHUNI WAIBA NG'OMBE KWA KUTUMIA PIKIPIKI

...

Baadhi ya Madiwani katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamelalamikia kuwepo kwa matukio ya wizi wa mifugo, kunakofanywa na baadhi ya wananchi katika Wilaya hiyo, hali inayopelekea baadhi ya wananchi kutojikita zaidi kwenye shughuli za maendeleo, badala yake wanakesha kulinda mifugo yao.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, baadhi ya Madiwani hao wamesema watu hao wamekuwa wakiwabeba ng'ombe kwenye bodaboda na kukimbia nao vijiji vya jirani.

"Hatuwezi kujadili maendeleo wakati kuna vitendo vya kihalifu vya wizi wa mifugo na haipiti siku hujasikia mifugo haijaibiwa kwenye eneo hili, kinachoshangaza zaidi ni wezi wanaiba ng'ombe na wanawabeba kwenye pikipiki, lazima tufanye kitu kwa niaba ya wananchi wetu." amesema Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Porini

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurudin Babu, ameagiza Kijiji kitakachobainika, kuiba ng'ombe basi wananchi wake hawana budi kuingia gharama ya kulipa ngombe hao.

"Nimeshaagiza tayari endapo Ng'ombe wataibiwa kwenye Kijiji fulani, wafuatilie nyayo na endapo watabaini hadi Kijiji alipoelekea huyo ng'ombe basi hicho Kijiji kitalazimika kulipa." amesema Nurudin Babu
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger