Tuesday, 27 August 2019

Wimbo wa TETEMA Wa Rayvanny na Diamond Platnumz Wapigwa Marufuku Kenya

...
Wimbo Tetema wa msanii Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz umepigwa marufuku kupigwa katika maeneo ya wazi  nchini Kenya.

Mbali na Tetema, wimbo mwingine uliopigwa marufuku kupigwa maeneo hayo ni  Wamlabez wa msanii Sailors wa nchini Kenya.


Kiongozi wa  Bodi ya Filamu nchini Kenya (KFCB),  Ezekiel Mutua amesema sababu ya kuzizuia nyimbo hizo  ni  kuwa na maudhui yanayokwenda kinyume na maadili.

"Nyimbo za Tetema na Wamlambez zinazuiwa kuchezwa nje ya vilabu na baa. Inatia aibu kuwaona hata viongozi wa kitaifa wakidensi na kuimba nyimbo za aibu mbele ya hadhara.

"Maneno katika nyimbo hizo ni uchafu na hayafai kusikilizwa hadharani hususan mahali ambapo kuna watoto wanaoweza kuwa wanasikiliza maneno au kuona mtu akicheza. Nyimbo zote mbili ni ponografia halisi ," ameandika bwana Mutua.

"Japo hatuzipigi marufuku kwasababu zinaimbwa kwa mtindo wa mafumbo , ni muhimu kwa umma kufahamu kuwa nyimbo hizi ni chafu, na hazifai kuchezwa mahala penye mchanganyiko wa watu wa rika tofauti. Acha zipigwe kwenye vilabu , kwa ajili ya watu wazima pekee !" aliandika.

Hata hivyo haijafahamika ni vipi agizo la Bwana Mutua litatekelezwa na bodi ya udhibiti wa maudhui ya kiusanii.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger