Thursday 29 August 2019

AJIUA KWA KUNYWA SUMU BAADA YA KUMUUA MKEWE KISHA KUMLAZA KITANDANI KAGONGWA

...
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard  Abwao
Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwanaume aitwaye Paschal Clement Mahona (32) mkazi wa Iponya kata ya Kagongwa wilaya ya Kahama amejiua kwa kunywa sumu baada ya kumuua mkewe Ashura Paschal (30) kwa kumnyonga shingo kisha kumlaza kitandani.


Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard  Abwao tukio hilo limetokea Agosti 28,2019 majira ya saa moja usiku.

"Ashura Paschal ambaye ni mkazi wa Iponya alikutwa akiwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na kulazwa kitandani na mmewe aitwaye Paschal Clement Mahona mbaye naye baada ya kufanya mauaji hayo alijiua kwa kunywa sumu ambayo aina yake bado kujulikana na kukutwa chumbani akiwa amelala sakafuni, akitoa povu mdomoni",amesema Kamanda Abwao.

"Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani  kabla ya tukio hilo wanandoa hao walikuwa wakigombana huku mume akimtuhumu mkewe kukosa uaminifu katika ndoa yao",ameongeza Kamanda Abwao.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger