Saturday, 31 August 2019

Polisi Pwani Yakamata Shehena Ya Vipodozi Feki

...
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi mkoani Pwani, linamshikilia Albert Kiwia (45) mkazi wa Kimara Dar es salaam kwa kosa la kusafirisha shehena ya vipodozi feki mbalimbali ,kwa kutumia gari aina ya Toyota Nissan.

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limefanikiwa kukamata madumu saba ya mafuta ya diezel yakiwa na ujazo wa lita 20 kila moja mali inayodhaniwa kuwa ni ya wizi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari kuwa ,mtuhumiwa huyo amekamatwa agost 29 mwaka huu, katika eneo la Mizani ya zamani -Kibaha Mji .

Alifafanua, licha ya tuhuma hiyo ya kusafirisha vipodozi hivyo ,jeshi hilo likamtaka aonyeshe kwa TRA stakabadhi alizolipia ushuru katika mipaka ya nchi wakati akiingiza vipodozi na hakuwa navyo

Aliwataka ,wafanyabiashara wenye tabia ya kuingiza bidhaa zao nchini kwa kukwepa kulipa kodi ,kuacha mara moja .

Wankyo alisema ,wamedhibiti mianya yote kwa wale wanaojaribu kukwepa kulipa kodi katika barabara zote za mkoa na wale watakaokamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hata hivyo, akielezea kuhusiana na tukio la kukamatwa madumu ya mafuta ya diezel ,alisema madumu hayo yamekamatwa ,eneo la Misugusugu ,Kibaha baada ya mtu aliyekuwa na mafuta hayo kuyatelekeza na kukimbia baada ya kuona gari la polisi likielekea mahali alikokuwa .

Wankyo alitoa wito kwa jamii kuacha kuhifadhi madumu ya mafuta aina ya diezel na petrol ndani ya nyumba kwani ni hatari.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger