Friday 30 August 2019

WAUMINI WASUSIA IBADA WAKIDAI PASTA MGENI BADO MBICHI HAJAOA 'ATAHARIBU BINTI ZAO'

...
Kisanga cha aina yake kimezuka katika kanisa moja la Gachororo, kaunti ya Kiambu nchini Kenya baada ya washirika kukosa kuhudhuria ibada wakidai pasta mgeni aliyetumwa kuwahudumia hakuwa na mke. 

Kondoo hao walisema kwamba, mtumishi alikuwa barobaro mwenye umri mdogo na kudai huenda alikuwa na njama fiche kanisani humo. 

Kwa mujibu wa Taifa Leo, washirika hao walianza kuondoka kanisani mmoja baada ya mwingine pindi tu mtumishi huyo aliposimama na kujitambulisha. 

Penyenye zinaarifu kwamba washirika hao walielezea wasiwasi wao kuhusu umri mdogo wa pasta kwani walihofia huenda akawa tishio kwa mabinti zao.

"Hata hajaoa. Mabinti zetu wataponea kweli. Huyu hapana. Huyu ni pasta hatari," washirika walisikika wakiteta.

 Inasemekana, pasta alijaribu kuwatuliza washirika hao na kuwaambia nia yake pale ilikuwa ni kueneza ijili ya Bwana na wala sio mambo mengine.

"Hayo hayawezekani. Nyinyi ni kama mnafanya biashara na kanisa. Rudi kwenu ukomae kwanza," mshirika mmoja alimfokea mchungaji. 

Duru zinaarifu kwamba, mtumishi huyo alikuwa amepewa uhamisho hadi tawi la kanisa hilo na kutoka alikokuwa akihubiri. 

Jaribilo la wazee wa kanisa kutuliza hali lilizua mzozo mkali huku waumini wakiwafokea na kuwataka kumshauri barobaro huyo kutafuta kazi nyingine ya kufanya na wala sio kuchunga kondoo. 

Penyenye zinaarifu kwamba, washiriki hao walimpa pasta muda wa siku mbili kusanya virago na kurejea alikotoka mara moja. 

 "Sisi hapa hatutaki kesi na wewe. Wasichana wetu wangali shuleni. Damu yako jinsi tunavyoiona ingali moto. Jipange uende kuhubiri kanisa lingine," waumini walizidi kumuonya pasta.

 Inadaiwa wazee walinza kuondoka mmoja baada ya mwingine na kumwacha pasta pekee yake baada ya kushindwa kudhibiti hali kanisani.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger