Sanamu ya mbao ya Donald Trump, iliyotengenezwa na Tomaz Schlegl, ilisimamishwa wiki kadhaa baada ya sanamu ya Melania Trump
Sanamu ya mbao ya rais wa Marekani imejengwa katika nchi alikozaliwa mkewe ya Slovenia, imeibua maoni tofauti.
Ikiwa na urefu wa karibu futi 26, sanamu hiyo ilijengwa katika ardhi ya kibinafsi na inamuonyesha Donald Trump akiwa na kichwa cha muundo wa mraba na kidevu huku akiwa anyenyenyua kichwa juu.
Msanii aliyeitengeneza amekiambia shirika la habari la AFP kuwa alitaka iwe kama kielelezo cha maoni ya kisasa ya wanaohisi kuwa watawala wa kisiasa hawawajali.
Sanamu hii imewekwa baada ya ile ya mke wa trump, Melania inayomuonyesha akiwa na ulimi uliojaa ndani ya mashabu.
Sanamu ya Melania, iliyochongwa ndani ya mti viungani mwa mji alikozaliwa wa Sevnica, inamuonyesha akiwa amevalia koti la rangi ya blu huku mkno wake ukionyesha angani. baadhi ya wakazi wanaichukulia kama ''aibu'', na wanasema inaonekana zaidi kama katuni kuliko mke wa rais wa Marekani.Mnara huu wa Trump unaripotiwa kujengw ana msanii wa Slovenia Tomaz Schlegl
Sanamu mpya ya rais wa Marekani ilijengwa katika kijiji cha Sela pri Kamniku, yapata kilomita 30 kusini -mashariki mwa mji mkuu wa Slovania -Ljubljana.
Mbunifu wake, Tomaz Schleglameliambia shirika la habari la AFP kwamba alilenga kutoa maoni ya wengi kupitia sanamu.
"Kwa mara ya kwanza ttangu Vita ya II ya dunia ndio mara ya kwanzamaoni ya wengi yanajitokeza kupinga utawala uliopo : Mtazame waziri mkuu wa Uingere za Boris Johnson, tazama Trump, rais wetu au waziri mkuu wa Hungary Viktor Orban. Dunia hii inaelekea wapi ?," alisema. "Tunataka kufungua macho ya watu kuelewa demokrasia ni nini ."
sanamu ya Bwana Trump inamuonyesha akiwa amevalia shati la blu na tai nyekundu, huku akiwa amesimama mithili ya mnara wa uhuru wa New York.
Bwana Schlegl anasema muundo wa ndani ya sanamu ya mbao unairuhusu kubadilika kutoka "sura ya urafiki mnamo siku za kazi za wiki na kuwa na sura ya kutisha sana katika siku za wikendi ", ikiwa ni sihara ya unafiki wa wanasiasa wanaotaka kuonyesha kuwa wanawajali wale wanaohisi kuwa wamesahaulika.
Lakini mnara huu umeibua maoni tofauti . Shirika la habari la AFP ililishuhudia mkazi mwenye hasira akiendesha gari lake la trekta na kugonga mnara huo wa sanamu wiki hii wakati maandalizi ya kuufungua rasmi Jumamosi yakiendelea.
Baadhi ya wakosoaji wa sanamu hiyo wamelalamikia juu ya "uharibifu wa mbao " na wakasema isingepaswa kujengwa .
"Majirani zetu wanadai sanamu hii ina sura mbaya na kwamba haifai katika eneo letu hili zuri tambalale ," Alisema Bwana Mr SchleglMnara huu wa Trump unaripotiwa kujengwa na msanii wa Slovenia Tomaz Schlegl
Watu wa Slovania wana maoni tofauti kumuhusu Rais wa Marekani . Mji anakotoka mkewe Mellania umekuwa ni kitovu cha utalii tangu alipochaguliwa mwaka 2016.
Huku wageni wakija kupata taswira ya mahali alikozaliwa na kuishi enzi za utoto wake , wakazi wametengeneza bidhaa zenye nembo ya melania zikiwemo kandambili, keki na baga zenye sura ya Trump na zilizopambwa na jibini iliyotengenezwa kama " nyweli" za Trump.
Japokuwa sanamu ya Mke wa rais ikiibua ukosoaji mwezi uliopita , mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP n kwamba kazi ya sanaa kuihusu lilikuwa ni " wazo zuri".
"Melania ni shujaa wa Slovenian , amefikia mafanikio ya juu nchini Marekani ," alisema Katarina, mwenye umri wa miaka 66.
Chanzo - BBC
0 comments:
Post a Comment