Saturday 17 August 2019

SERIKALI YAPONGEZWA KUTIMIZA AHADI YA UMEME BUSINDE - KIGOMA

...
Na Rhoda Ezekiel -Malunde1 blog Kigoma
Wananchi wa kata ya Businde Manispaa ya Kigoma Ujiji,mkoani Kigoma wameishukuru serikali kwa kuwatatulia kero ya muda mrefu ya umeme na kuomba shirika la umeme kuongeza nguzo ili waweze wananchi wote wanaohitaji huduma hiyo nao wapate umeme.

Wakizungumza jana wakati wa zoezi la ufunguzi wa Umeme wa REA  katika kata hiyo uliyozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga, Mwenyekiti wa mtaa wa Businde Husein Yaga alisema kwa muda mrefu wananchi walingoja kufikishiwa huduma hiyo na sasa serikali imetimiza ahadi yake ya kuwapatia umeme. 

Hata hivyo alisema  eneo lililopata umeme ni dogo,   hivyo kuliomba  Shirika la umeme kuongeza maeneo ya kuunganisha umeme ili wananchi wote wapate kuunganishiwa umeme  hasa katika maeneo ya taasisi za dini na sokoni.

Naye Diwani wa kata ya Businde Masoud Masoud aliomba  Shirika la Umeme (TANESCO) kuwaongezea nguzo 76 ili waweze kuunganisha umeme kwa asilima 80% katika eneo hilo kwani wananchi wengi wanahitaji wa umeme.

Meneja  wa TANESCO Mkoa wa Kigoma  Masangija Lugata, aliwataka wananchi ambao nyumba zao sio kubwa kutumia kifaa cha Umeta  ambacho gharama yake ni shilingi elfu 27 pamoja na elfu 32 ya vifaa vingine ili kuepuka gharama na usumbufu wa wakandarasi katika uvutaji wa umeme.

Alisema Serikali ilitoa maelekezo Businde ipatewe umeme, kiasi cha shilingi  Milioni  122  zilitolewa kwaajili ya kukamilisha zoezi la umeme wa  kilovoti 21 na kuunganishia  wateja waawali 156  ambao wamefungiwa umeme katika kata ya Businde. 

Alisema baadhi  ya wananchi wamefanyiwa mchakato wa kupatiwa umeme na utaratibu wa kuunganisha umeme unaendelea.

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga, alisema aliahidi kutatua kero ya umeme katika kata hiyo na alizingumza na viongozi wanaohusika na kero hiyo na tayari imetatuliwa, hivyo Tanesco wanatakiwa kuongeza nguzo ili wananchi wote waweze kunufaika na huduma hiyo.

Alisema kitu kikubwa kinachochochea maendeleo ni umeme hivyo ana uhakika baada ya wananchi kupata umeme huo, wataanzisha shughuli mbalimbali ili waweze kujikwamua na umaskini.

Aidha kuhusu changamoto ya maji ambayo ni kero nyingine, aliahidi serikali itatauta kero hiyo kabla ya mwezi wa kumi na moja maji yataaanza kutoka katika kata ya Businde na kuepukana na changamoto ya ukosefu wa maji.
Meneja wa TANESCO Kigoma Masangija Lugata akionyesha Wananchi kifaa cha Umeta kinachotumia gharama kidogo katika kuunganisha umeme.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga  akiwa na Meneja wa TANESCO Kigoma Masangija Lugata  na Diwani wa Kata ya Businde  wakati wa uzinduzi wa Umeme Businde
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger