Thursday, 8 August 2019

Rais wa Venezuela asitisha mazungumzo na upinzani kutokana na vikwazo vya Marekani

...
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameilaumu Marekani kwa vikwazo ilivyoiwekea nchi hiyo na kuamuru wawakilishi wa serikali yake kutosafiri kuelekea Barbados kwa mazungumzo yaliyopangiwa kufanyika na wanasiasa wa upinzani. 

Taarifa ya serikali ya Venezuela imesema Maduro ameamua kutowatuma maafisa wake kwa mazungumzo hayo yaliyopangiwa kufanyika leo Alhamis na kesho pamoja na kiongozi wa upinzani Juan Guaido kutokana na uchokozi mkubwa unaoendelezwa na utawala wa rais Trump. 

Rais Trump ameagiza kufungiwa kwa mali zote za serikali ya Venezuela zilizoko Marekani na pia amezuia kufanyika kwa biashara ya aina yoyote na uongozi wa nchi hiyo.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger