Friday, 2 August 2019

Marekani Yamuwekea Vikwazo Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania

...
Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Brigedia Jen. Mstaafu, Anselem Sanyatwe amewekewa vikwazo  na Marekani kufuatia kuhusika katika vifo vya raia 6 waliokuwa wakiandamana Agosti 2018 kushinikiza kutangazwa matokeo ya uchaguzi. 

Hata hivyo, Zimbabawe imeleza kutofurahishwa na  hatua hiyo  ya Marekani kumuekea vikwazo Anselem  Sanyatwe

Katika taarifa yake, serikali ya Harare imeitaja hatua hiyo ya Marekani kama inayodunisha uhuru wa taifa hilo na ambayo inashinikiza migawanyiko badala ya kuidhinisha uponyaji wa taifa na maelewano.

Wizara ya mambo ya nje Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Balozi Sanyatwe, ambaye ni Brigedia mstaafu ya jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais, kutokana na kuhusika kwake katika ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Wizara hiyo Marekani imefafanua kuwa ina taarifa za kuaminika kwamba Anselem Sanyatwe alihusika katika msako mkali dhidi ya raia Zimbabwe ambao walikuwa hawakujihami wakati wa ghasia zilizozuka mnamo Agosti mosi mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu, uliosababisha vifo vya raia sita.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger