Tuesday, 20 August 2019

Kizimbani Kwa Tuhuma Za Kumkata Msichana Sehemu Za Siri Kwa Wembe

...
Mkazi wa Tandale kwa Mtogole wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam,  Siasa Samwel (30) amepandishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jana Jumatatu Agosti 19, 2019 kwa tuhuma za kumkata msichana sehemu za siri na kumsababishia maumivu.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumkata mwanamke huyo sehemu za siri Novemba 15, mwaka jana na kumsababishia kupoteza bikra yake.

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veronica Mtafya, amedai tukio hilo lilitokea eneo la Tandale Chama Wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amekana shtaka hilo ambapo mwendesha mashtaka alidai upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kusomwa kesi hiyo.

Hakimu Lihamwike amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho na kusaini bondi ya Sh milioni moja.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya hayo na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapokuja kusomwa tena Septemba 2, mwaka huu.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger