











Na Dixon Busagaga wa Michuzi TV .
MBUNGE WA Jimbo la Vunjo ,James Mbatia ameshauri kuanzishwa kwa Utalii wa Tiba (Medical Tourism) katika eneo linalozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ili kurahisha utoaji wa huduma kwa wageni wanaopata matatizo wakati wa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mbatia aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi rasmi wa Hospitali ya St Monica iliyopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika kijiji cha Marua ,kata ya Kirua Vunjo Magharibi,katika wilaya ya Moshi huku akiiomba serikali kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara.
Akizungumza mara baada ya kufungua na kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali Hospitali iliyojengwa na Taasisi ya Kirua Children Care Foundation Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira ameipongeza taasisi hiyo kwa kujenga Hosptali hiyo ambayo itasaidia kupunguza changamoto za kiafya kwa wakazi wa maeneo hayo na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.
.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kirua Children Care Foundation Padri Amedeus Macha amesema Hospitali hiyo itakayo kuwa na uwezo wa vitanda zaidi ya 100 imelenga kutoa huduma za matibabu kwa wazee na watoto ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.
Dkt.Bogias Mwamgunda ni mwakilishi wa mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro hapa akaeleza namna ambavyo Hosptali hiyo itasaidia Wazee na watoto katika kupambana na magonjwa yatokanayo na Baridi .
Taasisi za Dini katika jimbo la Vunjo zimekuwa mstari wa mbele katika uwekezaji wa masuala ya huduma za afya ,hali inayochangia urahishaji wa upatikanaji wa matibabu tofauti na ilivyokuwa kwa kutembea umbali mrefu hasa nyakati za mvua na usiku .
Mwisho
|
0 comments:
Post a Comment