Thursday, 1 August 2019

CCM yashinda katika Uchaguzi wa Naibu Meya na Kaimu mwenyekiti wa Halmashauri mkoani Shinyanga

...
NA SALVATORY NTANDU
Diwani wa kata ya Igunda Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Makamo mwenyekiti wa Halmashauri hiyo katika Uchaguzi wa ndani wa  cha Chama cha Mapunduzi (CCM) kilichofanyika jana.

Uchaguzi huo umefanyika jana katika ofisi za CCM wilaya ya kahama ukiongozwa na Mwenyekiti wa uchaguzi huo Emmanuel Mbamange  ambaye pia ni katibu wa CCM wilaya ya Kahama na kusema kuwa mh, Katoto amepata kura 20 za ndio kutoka kwa madiwani wa Halmashauri hiyo waliohudhuria uchaguzi huo.

Amesema Halmashauri hiyo ina jumla ya madiwani 28 wa CCM lakini waliopiga kura ni 20 huku wengine wakiwa na udhuru mbalimbali na kusema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Mh, Katoto amewashukuru madiwani wenzake na kuahidi kutoa ushirikiano kwao ili kuhakikisha Halmashauri ya Ushetu inapata maendeleo.

Katika Hatua nyingine  Diwani wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga John Kisandu (CCM) amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, na kumshinda mpinzani wake Zena Gulamu (Chadema).


Uchaguzi huo wa Naibu Meya umefanyika jana kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani wa kumchagua Naibu Meya pamoja na Kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Manispaa hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi, elimu na afya, miundombinu, ukimwi, maadili pamoja na Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema John Kisandu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 15, dhidi ya mpinzani wake Zena Gulam kutoka Chadema ambaye amepata kura tano ,ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 20.

Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, Kisandu ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao na kuwa kitu kimoja katika kuisimamia halmashauri kwa maslahi mapana ya wananchi na kuwaletea maendeleo.

Aidha madiwani hao wameendelea kujadili ajenda mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, maji, miundombinu, fedha, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger