Thursday, 1 August 2019

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI BAADA YA KUUA BABA YAKE NA KUJERUHI WATU SABA KWA PANGA TARIME

...

Na Asha Shaban - Mara.
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Wambura Kisiri amemuua baba yake kwa kumkata kata kwa mapanga sehemu mblimbali za mwiliwake na kuwajeruhi watu wengine saba kwa panga katika sehemu mbalimbali za miili yao huko katika kijiji cha Kimusi kata ya Nyamwaga wilayani Tarime mkoani Mara.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 29,2019 majira ya saa sita na nusu mchana huko katika kijiji cha Kimusi Senta ambapo mtuhumiwa alitoka nyumbani kwake na kwenda nyumbani kwa baba yake mzazi huku akiwa na mapanga mawili mkononi na kufika na kuanza kumkatakata kwa mapanga mzazi wake huyo.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Tarime/Rorya Henery Mwaibambe alisema baba mzazi wa muuaji huyo anajulikana kwa jina la Kisiri Nyambari Kisiri alimaarufu Nyankongo (85)mkazi wa Kimusi aliuawa kwa kukatwa na panga kichwani,shingoni,tumboni na kwenye kiganja cha mkono wa kulia kwa kukiondoa chote.

"Aliuwawa kwa kukatwa panga na kijana wake ambaye baadae naye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kushindwa kutii agizo la polisi la kumta kuacha kufanya fujo ",alieleza.

Alisema baada ya kumkatakata kwa mapanga baba yake pia alimfuata shangazi aitwaye Rhobi Nyambari (38) ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa bega la kulia karibu na shingo,hali kadhalika kumjeruhi baba yake mdogo Marwa Nyambari (68) alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kichwani.

Mwaibambe aliongeza kuwa baada ya tukio hilo kuendelea alijitokeza mtu mmoja ambaye ni jirani Chacha Hura (29) kwenda kutoa msaada na bahati mbaya naye alikatwa panga mgongoni.

Aidha wakati tukio hilo likiendelea kutendeka mtuhumiwa huyo alijeruhi watu wengine wanne lakini hawakupata madhara makubwa na taarifa zilifika kituo cha polisi ambapo askari walifika eneo la tukio kwa kwa ajili ya kumkamata mtuhumiwa ambapo alitaka kuendelea kuwaua wananchi wengine.

Alisema askari polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto ndipo mtuhumiwa huyo alijeruhiwa kwenye nyonga kwa lengo la kumpunguza nguvu ili asiendelee kuleta madhara na kurahisisha ukamataji wake pamoja na kumnyang’anya silaha alizokuwa nazo.

Kamanda Mwaibambe alieleza kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kujeruhiwa alifariki dunia muda mfupi akiwa njiani kupelekwa hospitali ya wilaya ya Tarime kwa ajili ya kupatiwa matibabu na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Mwaibambe alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na polisi wanachunguza chanzo cha tukio hilo ambapo alisema majeruhi wote katika tukio hilo wamelazwa katika kituo cha Afya cha Muriba na halizao zinaendelea vizuri.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger