Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameamua kuahirisha ziara yake Mkoani Rukwa kutokana na ajali ya moto iliyotokea eneo la Msamvu Mjini Morogoro.
Ajali hiyo imetokea leo tarehe 10 Agosti, 2019 majira ya saa 2 asubuhi ambapo lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.
Waziri huyo ameanza safari kuelekea eneo la tukio.
0 comments:
Post a Comment