Saturday, 15 June 2019

Waziri wa Afya Autaka Uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuweka mashine kwa ajili ya kupimia ugonjwa wa Ebola

...
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameutaka uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuweka mashine kwa ajili ya kupimia ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 wakati akifanya ukaguzi kwenye uwanja huo kuangalia kama kuna mashine  za kupimia ugonjwa huo ambao umeripotiwa kuibuka nchini Uganda.

Amesema Serikali kupitia  wizara yake watatoa mashine kwenye kivuko cha Busisi, Kigongo na kituo cha mabasi cha Nyegezi jijini humo.

Pia,  kwa wasafiri hao wa mabasi kutoka nchi jirani wanaotumia mikoa ya Kigoma na Kagera.

"Kuwepo kwa Ebola sio tatizo hilo linaweza kuthibitiwa ila tatizo ni kusambaa kwa ugonjwa huo," amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake, kaimu meneja wa uwanja huo, Seneth Lyatuu amesema watatekeleza agizo hilo na wanahitaji mashine mbili kwa ajili ya abiria wa ndani na abiria wa nje.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger