Saturday 1 June 2019

WAVUTAJI SIGARA HATARINI KUSHINDWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

...

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani na Upasuaji Harisson Chuwa kutoka Hospitali ya Agakhan, amesema miongoni mwa madhara yanayosababishwa na matumizi ya Tumbaku ni wanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa kutokana zao hilo kuathiri zoezi la kusukuma damu mwilini.

Akizungumza kwenye kipindi cha Supamix cha East Africa Radio, Dr Chuwa amesema mbali na wanaume kudai mfumo wa maisha, ikiwemo lishe bora hupelekea kukosa nguvu za kiume lakini pia matumizi ya Sigara na mazao ya Tumbaku, hupunguza nguvu za kiume.

"Madhara mengine ya matumizi ya tumbaku inaweza kusababisha mwanaume kushindwa kushiriki tendo, kwa sababu mishipa ya damu inashindwa kufanya kazi vizuri, ndiyo maana tunasingizia tuna upungufu wa nguvu za kiume, lakini si kweli ni mfumo wa maisha tu wa uvutaji wa sigara" amesema Dr Chuwa.

Aidha Dr Chuwa amesema kuwa "moshi wa sigara una madhara kwa mvutaji mwenyewe na aliyekuwa naye karibu, madhara yanaanzia kwenye saratani ya mapafu, hii ndiyo saratani inayosababishwa na 95% ya matumizi ya sigara, ndiyo maana utakuta wake, waume au watoto wa watu wanaovuta sigara wanapata saratani hii"

Madhara mengine yanayoweza kutokana na matumizi ya tumbaku ni mtoto anapokuwa tumboni, moshi wa sigara unaweza kumuathiri kukua kwa mapafu yake, anaweza kupata pumu na mapafu yanaweza kujaa makamasi, na wakati mwingine inamfanya ashindwe kupumua.

Chanzo- EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger