MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wameanza utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kufanya mazoezi siku tatu kwa wiki baada ya muda wa kazi kuisha.
Mazoezi hayo hufanyika Jumanne, Jumatano na Ijumaa ambayo yameonekana kuwa chachu kwa watumishi ambao wamekuwa wakishiriki
Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi ya leo Kaimu Afisa Rasilimali Watu wa Tanga Uwasa Theresia Sanga alisema wameamua kufanya mazoezi hayo ili kuweza kuimarisha miili yao na kuiweka imara pia husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
Alisema pia kupitia mazoezi hayo mbali ya kuimarisha miili yao lakini pia yanajenga umoja na kuweka kujenga ushirikiano kwenye kazi hali inayosaidia kutekeleza majukumu yao vema.
“Lakini pia mazoezi yanaondoa msongo wa mawazo hivyo ni jambo zuri huku akiwahamasisha watumishi kuhakikisha kila wakati wanashiriki kwani yanafaida kubwa kiafya”Alisema
Awali akizungumza Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Dorrah Killo alisema mazoezi hayo ni mazuri kwa sababu yanawapa umoja na kupelekea kupendana ikiwemo kuongeza hari ya uwajibikaji.
0 comments:
Post a Comment