Hakimu katika Mahakama ya Wilaya ya Otuke huko Uganda Kaskazini Alhamisi iliyopita aliachwa na mshangao baada ya mtuhumiwa kuingia mahakamani hapo akiwa amevaa nguo zake zilizoibiwa ambapo kufuatia tukio hilo Hakimu alilazimika kuahirisha usikilizwaji wa kesi zote za siku ile kwa wiki moja kwa ajili ya kuimarika kutokana na mshtuko alioupata.
Imeelezwa kuwa mshukiwa huyo aliyeingia mhakamani hapo aliachiwa huru na jaji Benjamin Seruru tarehe 24 Mei baada ya kukutwa na hatia za kuiba mabegi, mtuhumiwa huyo Jimmy Oteng (34) mkazi wa Okelo katika kijiji cha Amone alikutwa na hatia za kuiba begi moja la ufuta kutoka nyumba moja huko Okelo mwaka 2018 na akahukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani.
Hata hivyo Mei 24 hakimu Seruru aliamua kumwachia huru baada ya kushindwa kupatikana kwa baadhi ya ushahidi dhidi yake.
Siku moja baada ya kuachiwa kutoka jela Oteng alifanya tukio la wizi nyumbani kwa hakimu huyo kwa kuiba suti jozi nne na nguo nyingine pamoja na madumu mawili ya lita 20 aliyodhani ni ya mafuta ya kupikia na alikamatwa siku ya jumatano wiki iliyopita.
Kamanda wa polisi wa Otuke alilieleza gazeti la Daily Monitor kuwa mtuhumiwa huyo amewahi kuiba katika nyumba mbili za watumishi wa mahakama ambao walieleza kuwa Oteng amewahi kuiba mafuta ya kupikia pamoja na vifaa vingine vya nyumbani na baadaye kwenda nyumbani kwa hakimu kufanya wizi huo.
Imeripotiwa kuwa Oteng amekuwa akifanya matukio hayo wakati mvua ikinyesha au wahusika wakiwa wameenda katika shughuli zao.
Imeelezwa kuwa baada ya kuiba katika nyumba ya hakimu alikutwa na wawindaji wawili amejificha katika kichaka huko Odugu katika kata ya Otuke ambao waliwaita polisi na akakamwatwa akiwa na vitu mbalimbali vilivyoibiwa katika nyumba ya hakimu zikiwemo suti jozi nne.
Kamanda wa polisi alieleza kuwa Oteng alifikishwa mahakamani siku ya alhamisi ambapo hakimu Seruru alihairisha kusikiliza kesi hiyo na kuamuru mtuhumiwa kubaki rumande hadi Juni 11 ambapo kesi hiyo itasikilizwa tena.
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
0 comments:
Post a Comment