Friday, 7 June 2019

MBUNGE AMUOMBA MMEWE AOLEWE NA MWANAUME WA PILI

...
Mjadala mkali umeibuka katika bunge la taifa la Kenya Alhamisi, Juni 6,2019 kufuatia kuteuliwa kwa mabalozi saba wa Kenya katika mataifa ya ng’ambo.


 Uteuzi wa Mwende Mwinzi, ambaye anashikilia uraia wa Kenya na Marekani, ndio ulikuwa ajenda kuu ya mjadala huo.

 Miongoni mwa viongozi waliomtetea vikali Mwinzi ni mbunge wa Mbita Millie Odhiambo ambaye alidai haoni hoja yoyote ya Mwinzi kuwa na uraia wa nchi mbili na bado ateuliwe kuwa balozi. 

Kulingana na mbunge huyo, atatangaza uraia wake endapo atakuwa na maafikiano na mumuwe amruhusu aolewe na mwanamme mwingine kando na yeye. 

Mbunge huyo ambaye ameolewa na Mzimbabwe, alidai kuwa bado anajadiliana na mumewe kuhusu kuolewa na mwanaume wa pili.

 "Mume wangu ni Mzimbabwe na sina uraia wa nchi mbili, kwa sababu bado niko kwa majadiliano na mume wangu aniruhusu niwe na mume wa pili," alisema Millie. 

Kulingana na mwanasiasa huyo, atabadilisha katiba na kutangaza uraia wake atakapopata ruhusa ya kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja.

 Kabla ya mjadala huo, wabunge walikubaliana kuwa kiongozi yeyote wa serikali hapaswi kuwa na uraia wa nchi mbili. 

 Kulingana na katiba kitengo cha 31(1) kuhusu uongozi na maadili, kiongozi wa serikali anayekabithiwa uraia wa pili hupoteza nafasi yake.

 Sheria hii inamlazimu Mwinzi kufutilia mbali uraia wake wa Marekani baada ya kuteuliwa kirasmi ili kuepuka kuvunja sheria. 
Chanzo - Tuko
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger