Wednesday, 19 June 2019

Mbunge Alalamikia Kushuka Biashara Kariakoo

...
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda na Biashara, Seleman Sadiqq, amesema  ukadirio wa kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na kutokuruhusiwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa China na Dubai kwenda na fedha taslimu umekuwa ni tatizo.

Akichangia mjadala wa Bajeti kuu ya Serikali  jana June 18 bungeni Sadiqq alisema tatizo lipo kwenye ukadiriwaji wa kodi na kwamba biashara za Dubai na China zimetawaliwa kwa kulipa fedha taslimu.

“Ni muhimu kwa Benki Kuu (BOT), ueleze utaratibu wa kupeleka fedha taslimu ukoje. BOT wasaidie kuhakikisha biashara inarudi Kariakoo, kwa sasa imepotea katika ramani ya biashara.

“Tulikuwa na Kariakoo ya wafanyabiashara kutoka Malawi, Kariakoo, Burundi, Congo, Uganda na Rwanda, BOT na TRA lazima wajiuelize kuna nini na sababu zipi tulizopoteza biashara Kariakoo,” alisema.

Aidha Mbunge huyo alisema sera ya Tanzania ya viwanda kwa sasa inatekelezeka kwa vitendo kutokana na ujenzi wa viwanda unaofanyika katika maeneo mbalimbali nchini.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger