Wednesday, 12 June 2019

Kiingereza kuendelea kuwa lugha ya kufundishia - Waziri Ndalichako

...
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce amesema Kiingereza kitaendelea kuwa lugha ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Akijibu swali la mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Athuman Maige leo, Ndalichako amesema Kiingereza kitaendelea kutumika kwa sababu ya umuhimu wake kitaifa, kikanda na kimataifa kwa mawasiliano na biashara ili kuwajengea wanafunzi ufahamu na umahiri wa lugha hiyo.

“Suala la matumizi ya lugha ya kufundishia na kujifunzia ni la kisheria kama ambavyo sheria ya elimu sura 353 inavyoelekeza. Sheria hiyo inabainisha matumizi ya lugha mbili za kufundishia na kujifunzia ambazo ni Kiswahili na Kiingereza.”

“Kwa sasa Kiswahili kinatumika kufundishia katika ngazi ya elimu ya awali na msingi, vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na vyuo vya ufundi stadi,” amesema Profesa Ndalichako.


Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger