Saturday, 8 June 2019

Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara atoa neno baada ya kutumbuliwa

...
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amesema alitarajia Rais John Magufuli kumuondoa katika wizara hiyo.

Amesema alilitarajia hilo kutokana na mazingira yaliyokuwa jana katika mkutano kati ya Rais John Magufuli na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini Tanzania uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Leo, Rais Magufuli amefanya mabadiliko  madogo katika baraza la mawaziri kwa kutengua uteuzi wa Kakunda na kumteua aliyekuwa naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Amesema kwa jinsi wafanyabiashara walivyotoa malalamiko yao Ikulu na kuinyooshea kidole Wizara ya Viwanda wakidai haiwatendei haki, kama kiongozi ilipaswa kujiuzulu.

Kakunda ambaye leo Jumamosi Juni 8, 2019 ametimiza siku 210 tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo akichukua nafasi ya Charles Mwijage ambaye pia aliondolewa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger