Friday 10 February 2017

Agizo wa Rais Magufuli uwanja wa ndege Dar laanza kutekelezwa

...
Shughuli za ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) jana tarehe 09 Februari, 2017 zimeendelea kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza jana tarehe 08 Februari, 2017.

Wafanyakazi 850 wameendelea na kazi mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kuingia na kushuka kwenye ndege, mifumo ya ujazaji wa mafuta ya ndege, maeneo ya kuegeshea ndege, sehemu ya kuingia na kutoka jengoni, mifumo ya viyoyozi na ujenzi wa nguzo.

Pia, timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi huo imefanyiwa mabadiliko ambapo wataalamu wengine 9 kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamepelekwa na kuanza kazi mara moja.

Mkandarasi ambaye ni kampuni ya BAM International ya Uholanzi, Mhandisi Mshauri ambaye ni kampuni ya ACE ya Misri na wafanyakazi walioajiriwa katika mradi huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua zilizowezesha shughuli za ujenzi kuendelea.

Katika ziara ya juzi, Mhe. Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na utekelezaji wa mradi huo uliopangwa kugharimu Shilingi Bilioni 560 kiasi ambacho ni kikubwa mno ikilinganishwa na jengo linalojengwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa alikiri kuwepo kwa dosari na kuahidi kuchukua hatua.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali inafanya juhudi za haraka kutoa malipo ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri yaliyosababisha kusitishwa kwa ujenzi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger